Wabunge wapya
wakila kiapo cha uaminifu bungeni baada ya kuanza kwa kikao cha kwanza
cha mkutano wa kumi, mjini Dodoma leo. Kuanzia kushoto ni Dk Damas
Ndumbaro wa Jimbo la Songea Mjini, Justin Monko wa jimbo la Singida
Kaskazini na Dk Stephen Kisurwa wa Jimbo la Longido. Picha na Edwin
Mjwahuzi
Mkutano wa 10 wa Bunge umeanza Januari 30 mwaka 2018 mjini Dodoma kwa wabunge wapya watatu wa CCM kula
kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.
Wakati wabunge hao wakila kiapo, takribani wabunge 50 wa upinzani walikuwa nje ya ukumbi wa chombo hicho cha kutunga sheria.
Walioapishwa ni Dk Damas Ndumbaro (Songea Mjini), Justin Monko (Singida Kaskazini) na Dk Stephen Kisurwa wa Longido.
Pia, Dk Tulia aliomba wabunge kusimama
kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini, Leonidas
Gama ambaye alifariki dunia Novemba mwaka jana.
Na Habel Chidawali, Mwananchi
SHARE
No comments:
Post a Comment