Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kati April 9 na June 21, 2013.
Katika kesi hiyo ya jinai namba 25, 2018, Samaje ambaye pia alikuwa Katibu wa Bodi ya Ushauri wa Madini anadaiwa wakati akitimiza majukumu yake kwa makusudi alitumia vibaya madaraka kwa kushindwa kuitisha mkutano wa bodi hiyo na kupata ushauri wake.
Inadaiwa kuwa kuzingatia maombi ya leseni ya madini namba HQ-P26114 kwa ajili ya madini ya Gemstones and, Associated Minerals ikiwamo Graphite na Marble katika eneo la Merelani, Wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara ambayo iliwasilishwa na Kampuni za Tanzaniteone Mining Limited na M/S State Mining Corporation, kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 8(4) cha sheria ya madini namba 14 ya 2010 kwa lengo la kuzipatia faida ya eneo la madini la Kilometa 7.6 kwa makampuni hayo.
Kosa la pili, Swai amedai kuwa Samaje April 16,2013 alitumia vibaya madaraka yake kwa kutoa maelekezo kwa Kamishna Msaidizi wa leseni na Haki za Madini, John Nayopa kuandaa leseni za kuchimba madini ya Gemstones ikiwamo Tanzabite, Graphite na Marble bila ya kuzingatia mfumo wa uendeshaji wa taarifa za madini wa Cadastie (MCIMS) wa Wizara ya Nishati na Madini wa eneo la Kilometa 7.6 Mererani Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.
Kitu ambacho ni kinyume na kifungu cha 49 (2) (b) cha sheria ya madini namba 14 ya 2010 na kusababisha Kampuni hizo kupata faida ya leseni za kuchimba madini.
Baada ya kusomewa Mashtaka hayo, Samaje ambaye anatetewa na Wakili Jema Bilegea alikana na upande wa Mashtaka aumedai kuwa upelelezi umekamilika.
Hakimu Nongwa alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili wenye anuani za kuaminika ambapo kila mdhamini asaini bondi ya shilingi Milion 50.
Pia mshtakiwa huyo asitoke nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha Mahakama, mshtakiwa akitimiza masharti hayo kwa kudhaminiwa na Mhandisi wa Migodi Mwandamizi, Zephania na Mhasibu Mwandamizi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, Donald.
Kesi imeahirishwa hadi Februari 28,2018 ambapo mshtakiwa atasomewa maelezo ya awali (PH).
SHARE
No comments:
Post a Comment