Makamu rais wa
Marekani, Mike Pence amegoma kuwepo katika chakula cha jioni ambacho
alitakiwa kukaa meza moja na kiongozi wa serikali ya Korea Kaskazini
Kim Yong-nam.
Wakati huo huo, rais wa Korea ya Kusini Moon Jae-in ameshikana mikono na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un katika sherehe za ufumbuzi wa mashindano ya michezo ya Olympiki ya msimu wa baridi.
Michezo hiyo inaendelea wakati ambapo kuna mvutano juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Pence alimleta Fred Warmbier kama mgeni Korea Kusini, baba wa kijana mdogo wa Marekani aliyekufa baada ya kutolewa gerezani huko Korea Kaskazini.
Bwana Pence na Kim Yong-nam walikuwa wenyeji wa rais wa Korea Kusini kabla ya sherehe haijaanza huko Pyeongchang.
Lakini Makamu rais wa Marekani alikaa kwenye tafrija hiyo kwa dakika tano tu na kuondoka.
Katika shughuli hiyo, Bwana Moon alisema anatarajia mashindano hayo ya michezo ya Olimpiki msimu wa baridi yataweza kukumbukwa kama siku nzuri ya kuanza kuwa na amani.
Hata hivyo ziara yake inaonekana kuwa ishara kwamba Kim Jong un yuko tayari kuimarisha uhusiano na Korea Kusini ,nchi ambazo zilikuwa katika mvutano kwa kipindi kirefu.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment