Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) na Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony
Mavunde (Kulia) wakifatilia taarifa ya Mkoa wa Shinyanga mara baada ya
kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi, tarehe 27 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Bi Haula Kachwamba akizungumza
jambo mara baada ya Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka
Biteko (Kulia) na Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony
Mavunde (Kushoto) kuzuru katika ofisi za chama wakiwa katika ziara ya
kikazi.
Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo mara baada ya kuwasili Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi akiwa sambamba na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde.
Na Mathias Canal, Shinyanga
Naibu
Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko na Naibu Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde, tarehe 27
Februari 2018 wametinga Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ya siku
moja ambapo pamoja na mambo mengine watatembelea mgodi wa EL-Hillal Minerals Ltd.
Mhe
Biteko ametinga Mkoani Shinyanga akitokea ziarani Mkoani Tabora huku
Mhe Mavunde akiwa ametokea Mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji
wa maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi mwaka
2015-2020.
Wakati
Mhe Mavunde akiwa kwenye ziara ya kukagua Viwango vya Kazi na Usajili
wa waajiri kwa mfuko wa fidia wa wafanyakazi (WCF) ni sehemu ya kukagua
Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa agizo la Mhe Jennister
Mhagama ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na
Ajira ambaye aliwataka waajiri wote nchini wawe wamejisajili kwenye
mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2017.
Amesisitiza
waajiri kujisajili na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kwani kutofanya
hivyo Kwa mujibu wa Kifungu cha 71(4) atashitakiwa Mahakamani na
akikutwa na hatia adhabu yake ni faini isiyozidi TSh 50,000,000 au
kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja.
Wakati
huo huo Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesisitiza
umuhimu wa wachimbaji wadogo nchini kulipa kodi huku akieleza kuwa
wachimbaji wanapaswa kujiunga kwenye vikundi kwani serikali imetenga
maeneo mengine ambayo itatoa wataalamu kuyafanyia Utafiti ili kuimarisha
uchimbaji nchini kwa wachimbaji wadogo kuwa wenye tija na hatimaye
kuwafanya kutoka katika uchimbaji mdogo kufikia wa kati na hatimaye kuwa
wachimbaji wakubwa.
Pia
ameendelea kusisitiza juu ya Wamilili wa Leseni za Madini kote nchini,
kutunza takwimu za gharama za uendeshaji wa shughuli zao za uchimbaji na
kila Mwezi ziwasilishwe kwa Afisa Madini kwani kutokufanya hivyo
wataingia katika mikono ya sheria kwa kulipa faini ya shilingi milioni
50 mpaka milioni 150 au kifungo cha mwaka mmpja jela.
Pia,
Mhe Biteko ameeleza dhamira ya ziara yake kuwa anapokuwa katika maeneo
mbalimbali anawakumbusha wachimbaji nchini kufuata sheria na taratibu za
nchi.
MWISHO.
SHARE
No comments:
Post a Comment