TRA

TRA

Tuesday, February 27, 2018

MTUNZI WA WIMBO WA “TANZANIA YETU NI NCHI YA KUPENDEZA” AMELAZWA MUHIMBILI ANAHITAJI MSAADA WA MATIBABU

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Mtunzi wa wimbo wa TANZANIA YETU NCHI YA KUSIFIKA, Steven Hizza anahitaji msaada
MZEE Stephen Hizza (kama anavyoonekana pichani), ambaye ni mtunzi na mwimbaji wa wimbo maarufu wa TANZANIA YETU NI NCHI YA KUPENDEZA, amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, na anahitaji msaada ili kumudu matibabu.
Mzee Hizza amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wodi ya Kibasila namba 14 akiugua ugonjwa wa tezi dume. Anawaomba Watanzania kumpa msaada wa kifedha ili kumudu hali yake ya kuugua. Kama unaweza kumtumia kiasi chochote cha fedha tume kupitia namba ya simu 0657-513067.

Wimbo wa TANZANIA YETU
Wimbo huo aliutunga na kuuimba mwaka 1966 akiwa na bendi ya Atomic Jazz ya mkoani Tanga, wakati huo taifa likiwa limefikisha miaka mitano tu tangu kupate Uhuru mwaka 1961.
Mwandishi wa habari hii anasema alifanya mahojiano naye mwaka 2011 kwa kumfuata Jiji la Tanga wakati wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kupata Uhuru wa iliyokuwa Taganyika.
“Hakika mzee huyu ni HAZINA yetu kutokana na utunzi wa wimbo huo ambao unahamasisha uzalendo na kuipenda nchi yetu,” ameeleza mwandishi Yusuph Mussa, anayeripoti kutokea Korogwe, mkoani Tanga
Habari kwa hisani ya Immamtukio blog

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger