WAHITIMU waliosoma Shule ya Sekondari Kilakala ,
iliyopo mkoani Morogoro wameombwa kujitokeza kuunga mkono mpango wa
Serikali wa uimalishaji wa miundombinu ya elimu itakayoweka mazingira
mazuri yatakayowavutia wanafunzi kusoma.
Rai hiyo imetolewa na wahitimu wa mwaka wa masomo 1986 hadi 1995 ambao wameanzisha umoja wao ukiwa na lengo la kusidia utatuzi wa changamoto mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa huduma za afya kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Muhitimu
wa zamani wa shule hiyo , Wanyenda Kuta , aliyeambatana na wenzake
15 waliosoma kwenye hiyo ya wasichana wenye vipaji maalumu , Augosti
27, mwaka huu alisema, shule ya Kilakala imetoa wahitimu wengi wanawake.
Alisema ,
asilimia kubwa ya waliohitimu katika shule hiyo ni watumishi katika
ngazi mbalimbali za Kiserikali , Viongozi wa kisiasa , Mashirika ya Umma
, Sekta binafsi na wajasilimali wakubwa .
Hivyo
alisema , wao walipita katika mikono salama ya shule, walimu
,wazazi na Serikali na kwa sasa wanao wajibu wa
kurudisha kidogo wanachokipata kwa kusaidiana na Serikali
kwenye mpango yake ya kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo katika
shule hiyo.
“
Kufika kwetu hapa kumetokana na wananchi kulipa kodi za Serikali
ambayo ilijenga shule hii ambayo imetuwezesha sisi kupata elimu bora
hapa Kilakala” alisema Kuta.
Hivyo
alisema , kwa kutambua umuhimu huyo, wahitimu hao waliamua
kuchangishana fedha na kupatikana kiasi cha Sh milioni
tatu zilizosaidia kununua shuka, magodoro na ukarabati wa Zahanati ya
Shule ili hiyo.
Pamoja
na hayo ,alitumia nafasi hiyo kuwasihi wanafunzi wakike wanaosoma
katika shule hiyo wajitambue kuwa wanaowajibu nao kuja
kulisaidia taifa lao kwa vile Serikali inatumia kodi za wananchi
katika kuboresha mazingira ya elimu nchini.
“ Kilakala Sekondari
imetoa na itaendelea kutoa wataalamu wa fani mbalimbali nchini ,
na wale ambao ni matunda ya shule hii tuangalie tulikotoka “ alisema
Kuta na kuongeza kuwa.
“
Jambo ambalo tunaweza kulifanya ni kuchangia kuboresha shule yetu
ikiwezekana kuanzisha siku maalumu kwa wote waliosoma hapa ili michango
yetu isaidia kuboresha shule hii , tunao baadhi ya viongozi wa ngazi
za juu serikalini wakiwemo mawaziri ” alisema Kuta.
Kwa
upande wake Kiranja mkuu wa shule hiyo, Gema Kataraiya, pamoja na
Kiranja wa Afya kwa nyakati tofauti waliwapongeza wahitimu hao kwa kutoa
mashuka na kukarabati jengo la Zahanati ya shule hiyo'
Pamoja
na ukarabati wa Zahanati hiyo, wanafunzi hao walisema bado kuna
upungufu mkbwa wa vifaa vya kutolea huduma vikiwemo vipimo vya malaria
na mazingira yasiyo rafiki ya vyoo.
Awali, Makamu
Mkuu wa Shule hiyo upande wa Taaluma, Mussa Katunzi, alisema kuwa
mchango uliotolewa na wahitimu hao ni moja ya chachu ya kuwavuta wengine
aliosoma shule hiyo kuona nao wanaowajibu wa kuchangia maendeleo ya
elimu .
Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala ,
inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda umoja wao wakiimba wimbo wa
shule ikiwa ni ishara ya kukumbuka walipokuwa wanafunzi shuleni
hapo baada ya kufika shuleni hapo Augosti 27, mwaka huu kukabidhi
msaada shuka na madogoro kwa ajili ya Zahanati ya shule ambayo pia
ilikarabatiwa na michango yao.
.............................. .
Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda umoja wao wakiekelea jengo la Ofisi ya Mkuu wa shule kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni.
Mhitimu wa shule ya Sekondari Kilakala , Claudia Iringo akimkaabidhi mwanafunzi wa shule hiyo madafyari kwa ajili ya wenzao wenye mahitaji maalumu , wahitimu hao wa zamani wapatao 15 waliosoma kuanzia 1988 hadi 1995 waliitembele shule yao Augosti 27, mwaka huu .
Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda umoja wao wakiwa katika Ofisi ya Mkuu wa shule kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni wa shule baada ya kufika shuleni hapo Augosti 27, mwaka huu kukabidhi msaada shuka na madogoro kwa ajili ya Zahanati ya shule ambayo pia ilikarabatiwa na michango yao.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala,inayomilikiwa na Serikali wakifurahia kuona wahitimu wa zamani katika shule hiyo wamewakumbuka kwa kutoa kmsaada shuka na madogoro kwa ajili ya Zahanati ya shule na kulikarabati jengo hilo.
Picha ya pamojana mwalimu na viongozi wa wanagfunzi
Wahitimu wakiangalia shughuli za shule yao
Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda umoja wao wakiimb na kicheza kukumbusha enzi zao katika shule hiyo.
Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda umoja wao pamoja na baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa shule hiyo, walimu na bodi ya shule wakiwa ndani ya jengo la zahanati ya shule baada ya kukabidhi shuka, magodoro pamoja na madatfari kwa wanafunzi.
SHARE
No comments:
Post a Comment