Rais mpya wa Liberia George Weah amemfuta kazi Waziri wa sheria Charles Gibson, baada ya malalamishi kuwa amepokonywa leseni ya uwakili baada ya kumtapeli mteja wake. Kabla ya uteuzi wake, Gibson alipatikana na hatia hiyo na Mahakama ya Juu baada ya kumtapeli mteja wake Dola za Marekani 25,000 na kuagizwa kuzirejesha.
SHARE
No comments:
Post a Comment