Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameivunja Kamati ya maji ya kata
ya Didia iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kutokana na
kufanya ubadhirifu kwenye mradi wa maji wa kisima kirefu.
Kamati
hiyo inadaiwa kutafuna pesa za mradi ulioanza kujengwa mwaka 2013/2014
na kukabidhiwa mwaka 2016 na kugharimu shilingi milioni 400.16
umeshindwa kuendelea kuhudumia wananchi mara baada ya kifaa kimoja
kuharibika na kukosekana pesa za matengezo na kuufanya mradi kutaka
kufa.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Didia jana Februari
8,2018 mkuu wa wilaya aliamua kuvunja kamati hiyo na kuagiza wajumbe wa
kamati hiyo wakamatwe. “Kamati hii kuanzia sasa nimeivunja na ninaagiza
jeshi la jadi Sungusungu watu hawa watafutwe wakamate na wapelekwe
Polisi sababu ni wahujumu uchumi na kisha wapewe muda wa kizirudisha
pesa zote walizozitafuna kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria,”
alisema Matiro.
Hata
hivyo mara baada ya kuivunja kamati hiyo ya maji, alisimamia zoezi la
wananchi kuchagua viongozi wengine sita wa mpito kupitia mkutano huo wa
hadhara kwa kuchaguliwa na wananchi wakiongozwa na mwenyekiti wake
Katunge Njile, huku akiagiza viongozi wote wa vitongoji kuitisha
mikutano ya hadhara na kuchagua wajumbe wawili wawili ambao wataunda
kamati ya maji ya kudumu.
Pia
aliagiza kila kaya kwenye kata hiyo ya Didia yenye wakazi 4112 wachange
shilingi 3000, fedha ambazo zitasaidia kununua kifaa kwenye mradi huo wa
maji chenye gharama ya shilingi milioni 3.7, ili uanze kufanya kazi na
kuondoa adha ya wananchi kutumia maji machafu sambamba na kumtua ndoo
kichwani mwanamke.
Naye
aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya maji Selemani Msabaha, alikiri
kuwa walishindwa kuendesha mradi huo mara baada ya pesa kukosekana
ambapo mpaka sasa kwenye akaunti kuna shilingi 129,000. Kwa mujibu wa
mkaguzi wa ndani wa halmashauri hiyo Sumbukeni Malela kamati hiyo
ilikuwa ikikusanya hadi shilingi milioni 17 na walikuwa hawafanyi vikao
na hakuna listi za manunuzi ya vifaa vinapoharibika na kwamba kiasi cha
shilingi 984,600 hazijulikani zilipo.
Mkuu
wa wilaya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa Kata ya
Didia Shinyanga na kuivunja kamati ya maji kutokana na kufanya
ubadhirifu wa fedha na kukwamisha mradi huo kutofanya kazi tena. Picha
zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Wananchi wa kata ya Didia wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Aliyekuwa
mwenyekiti wa Kamati ya maji iliyovunjwa kata ya Didia Selemani Msabaha
akizungumza mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na
wananchi na kukiri mradi huo wa maji Didia kuwa umeshidwa kuendelea
kutoa huduma mara baada ya fedha za matengenezo Shilingi milioni 3.7
kukosekana
Mkaguzi
wa ndani wa halmashuri ya Shinyanga vijijini Sumbukeni Malela ,akieleza
jinsi ubadhirifu wa fedha ulivyotumika kwenye mradi huo wa maji
Didia.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
SHARE
No comments:
Post a Comment