Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi, watendaji
katika Sekta ya Afya pamoja na wadau mbalimbali wa Afya mkoani humo
katika kikao maalum kilichofanyika kwa lengo la kutathmini mchango wa
wadau wa Afya(mashirika mbalimbali yanayofanya kazi na mkoa huo) ambacho
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akifafanua jambo katika kikao
kati ya Viongozi wa Mkoa huo , watendaji wa Sekta ya Afya ngazi ya mkoa
na Wilaya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini
Bariadi.
Mratibu
wa Mpango wa Kudhibiti UKIMWI Mkoa wa Simiyu, Dkt.Khamisi Kulemba
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango huo Mkoani humo katika
kikao kati ya Viongozi wa Mkoa huo , watendaji wa Sekta ya Afya ngazi ya
mkoa na Wilaya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika
Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau
mbalimbali wa Sekta ya Afya Mkoani humo wakifuatilia mada mbalimbali
katika kikao cha tathmini ya mchango wa wadau mbalimbali wa Afya Mkoani
Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwakilishi
Mkazi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi
ya watu (UNFPA), Bi. Christine Mwanukuzi Kwayu akichangia jambo katika
kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na
wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirikala Cuso International Tanzania, Ndg.Romanus Mtung’e
akichangia jambo katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu ,
watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau
mbalimbali wa Sekta ya Afya Mkoani humo wakifuatilia mada mbalimbali
katika kikao cha tathmini ya mchango wa wadau mbalimbali wa Afya Mkoani
Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi.
Shekhe
wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola akichangia jambo katika kikao kati
ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa Sekta ya Afya na wadau
mbalimbali wa Sekta ya Afya kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Kikristo Mkoa wa Simiyu (CCT), Mchungaji Martine Samson
Nketo akichangia jambo katika kikao kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu ,
watendaji wa Sekta ya Afya na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu , watendaji wa
Sekta ya Afya na wadau (mashirika) mbalimbali wa Sekta ya Afya
wanaofanya kazi na Mkoa huo mara baada ya kufungua kikao kilichofanyika
Mjini Bariadi.
………………
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewataka wadau na mashirika
mbalimbali wanaofanya kazi na Mkoa huo katika sekta ya Afya kuelekeza
fedha zao zaidi katika masuala yanayojibu mahitaji ya wananchi wa Mkoa
huo kwenye Afya badala ya kujikita zaidi katika kugharamia mafunzo na
semina kwa watumishi.
Mtaka
ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika Februari 26, Mjini Bariadi
kwa lengo la kufanya tathmini ya mchango wa fedha za wahisani na wadau
mbalimbali wa sekta ya Afya mkoani Simiyu na matokeo yake katika
mahitaji halisi ya Kiafya kwa wananchi.
Mtaka
amesema mkoa huo una wadau wengi wanaounga mkono juhudi za Serikali
katika sekta Afya na wanatoa fedha nyingi ambazo zikiwekwa pamoja na
fedha zinazotengwa na Serikali kupitia bajeti za Halmashauri zinaweza
kujibu mahitaji ya mkoa huo ambayo ni pamoja na upungufu wa zahanati na
vituo vya Afya
“
Msingi mkubwa wa kikao hiki ni kutaka tufanye tathmini ya fedha
zinazotolewa na wadau ndani ya mkoa wetu, kwa mwaka huu kwenye
Halmashauri zetu tumetenga Bilioni 33.4 na tuna shilingi bilioni 11
kutoka kwa wadau kwa ajili ya sekta ya afya, hivi ‘impact’(matokeo) ya
hizi bilioni 11 iko wapi? Natamani hapa kila mwenye fedha yake atuambie
mwaka huu atafanya nini” alisema Mtaka.
“Nashukuru
TAMISEMI mko hapa hili ni la kuliangalia , kama tunaingia mikataba ya
shilingi bilioni 11 kwa mwaka na mashirika yanayofanya kazi za Afya
ndani ya Mkoa kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi, uhamasishaji na
semina, wakati tukiwa kwenye mazingira ambayo hatuna hata nusu ya idadi
ya zahanati na vituo vya afya vinavyohitajika ni lazima tutafakari wote”
alisisitiza Mtaka.
Wakati
huo huo Mtaka ametoa wito kwa wataalam wa Afya kuendelea kutoa elimu na
kuwahamasisha wananchi kuzingatia uzazi wa mpango na akasisitiza
umuhimu wa kutoa elimu kwa wazazi watarajiwa (vijana) ili waanze kufanya
maandalizi mapema juu ya maamuzi ya idadi ya watoto watakaoweza
kuwahudumia baadaye.
SHARE
No comments:
Post a Comment