Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akiteremka kwenye boti
katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga
bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda
iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani
Mbeya
Meneja wa
Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Sese (wa pili kushoto)
akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa
pili kulia) wakati wa ziara yake kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani
Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya. Wa kwanza
kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Deo Ngalawa na wa kwanza kushoto
ni Katibu wa Mhe. Nditiye Mhandisi Hamza Faiswary.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyeketi) akisimikwa kuwa
Chifu wa kitongoji cha Ihiiga kilichopo kwenye kijiji cha Nkwimbili,
kata ya Lupingu, Wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe ikiwa ishara ya
pongezi kwa kiongozi wa kitaifa kufika hapo tangu mwaka 1979 katika
ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari
kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo
wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya.
Wa kwanza kushoto ni mzee Thadei Otmari Ngalawa na aliyevaa miwani ni
Diwani wa Kata ya Lupingu Mhe. Skanda Mwinuka.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Nsele kilichopo kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Njombe
katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga
bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda
iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani
Mbeya
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa Mzee Kolimba akimshukuru Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati wa
ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari
kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda wilaya
ya Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya
………………….
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga shilingi milioni 358 kwa
ajili ya kulipa fidia nyumba na ardhi za wananchi waishio mwambao wa
Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari za
Ziwa hilo
Hayo
yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara
yake aliyoifanya ya kukagua bandari za Ziwa Nyasa kuanzia bandari ya
Manda iliyopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe hadi bandari ya Itungi
iliyopo wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.
Katik
ziara hiyo, Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri
Msese amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania imetenga fedha hizo kwa
ajili ya kulipa fidia wananchi wa maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa
waliojitolea maeneo yao ili kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari
zilizopo ndani ya Ziwa Nyasa kuanzia bandari ya Lipingu iliyopo Wilaya
ya Ludewa mkoa wa Njombe hadi bandari ya Matema iiyopo wilaya ya Kyela
mkoani Mbeya.
Naye Mkuu
wa Wilaya wa Ludewa Bwana Andrea Tsere amemueleza Mhandisi Nditiye kuwa
tayari wamekamilisha kazi ya kuhakiki malipo ya fidia za wananchi
waliotoa ardhi zao eneo la Manda na Lupingu. “Wanachi wa eneo la Manda
watalipwa shilingi milioni 192 ambapo wametoa eneo la ukubwa wa hekari
24 na wa Lupingu wametoa eneo ukubwa wa hekari 10.6 na watafidiwa
shilingi milioni 166, amesema Tsere”.
Bwana
Msese amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania inakamilisha ujenzi wa
meli ya mizigo na abiria na itaanza kazi ya kusafirisha abiria na mizigo
ndani bandari za Ziwa Nyasa mwezi Agosti mwaka huu ambapo meli hiyo
itakuwa na uwezo wa kubeba abiria mia mbili na mizigo tani mia mbili
kwenye jumla ya bandari kumi na tano zilizopo ndani ya mwambao wa ziwa
Nyasa.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Deo Ngalawa amemshukuru Mhe. Mhandisi
Nditiye kwa niaba ya wananchi wake kwa kufika kwenye makazi ya wananchi
hao waishio kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa na kukagua mahitaji ya usafiri
wa majini wa abiria na mizigo wa Ziwa hilo ambapo Serikali tayari
imetenga fedha kulipa fidia wananchi waliotoa maeneo yao kupisha ujenzi
na upanuzi wa bandari za Ziwa hilo.
Ujenzi wa
bandari hizo na utoaji wa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo ni
ukamilishaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kwa wananchi waishio kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa
ambao wanategema Ziwa hio kwa kiasi kikubwa kwa shughuli za kiuchumi,
biashara na kijamii ambazo zitachangia ukuaji wa uchumi wa wananchi hao
na taifa kwa ujumla.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano
SHARE
No comments:
Post a Comment