TRA

TRA

Friday, February 9, 2018

Wenger: Wachezaji wa Uingereza ni 'mabingwa' wa kujiangusha uwanjani

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amelalamika kwamba wachezaji wa Uingereza wamekuwa na tabia ya kujirusha na kutengeneza adhabu. 


Amesema mchezaji wa Tottenham Dele Alli alifanya kitendo hicho kwenye mchezo wa jumapili huko Liverpool na kusababisha mwamuzi kutoa adhabu ya penalti.

 Arsene Wenger alalama huu ni mchezo mchafu

Mchezaji mwingine ambaye anatuhumiwa kufanya kitendo hicho ni Harry Kane, alifanya hivyo kwa mchezaji Virgil van Dijk wa Liverpool na kusababisha mpira wa adhabu
Wenger amesisitiza kwamba anakumbuka kumekuwa na kesi za wachezaji kutoka nje ya Uingereza, lakini wachezaji wa Uingereza sasa wameiga tabia hiyo na wamekuwa vinara wa matukio hayo kuliko wachezaji wengine.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger