Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora amewataka
wafanyabiashara nchini kuhamasika kujiunga na mtandao wa mitaji ya ubia
ili kuimarisha vitega uchumi vyao na pia kusaidia kuanzisha viwanda hapa
nchini.
Profesa
Kamuzora alisema hayo wakati akizindua Mtandao wa Mitaji ya Ubia
Tanzania – Tanzania Venture Capital Network jijini Dar es salaam jana.Aidha
Katibu Mkuu huyo amesema uzinduzi wa mtandao huo umefanyika wakati
mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza
Tanzania kuwa nchi ya viwanda,
Aliwataka
wananchi kuacha uoga katika ushiriki wa kuwawezesha kuwepo kwa mitaji
ya kutosha kwa ajili ya uimarishaji wa uwekezaji nchini Tanzania.Alisema
serikali kwa sasa inafanya kila linalowezekana kuhakikisha mazingira ya
biashara na uwekezaji yanakuwa bora, ndio maana wameanzisha mchakato wa
kutengeneza sera ya maendeleo ya viwanda hasa katika sekta binafsi.
Alisema
ni vyema wenye viwanda na wananchi wengine kushiriki katika mchakato
huo ili kufanikisha nia ya kuipeleka Tanzania katika nchi ya viwanda.
Alisema kwa kuwa na sera sheria nyingi zitabadilika na hivyo kupunguza
urasimu na pia vikwazo vya kuwezesha kazi katika masuala ya viwanda na
biashara.
Pia alitaka wamiliki wa Ubia huo kushirikiana na Costech katika kuhakikisha kwamba viwanda vinaanzishwa na kuendelezwa.Alitaka kuwepo na elimu ya fedha na mitaji ili wananchi waweze kuthubutu na kufanikisha mitaji.
Mapema
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi
amewataka wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa uwazi, kwa kuzingatia
sheria za nchi, na kuwa tayari kujifunza maarifa mapya kila fursa
inapojitokeza.
Akisitikishwa
na mahudhurio duni ya wafanyabiashara katika hafla hiyo alisema
kutofahamu undani wa soko la mitaji na fursa zake kunatokana na kutokuwa
wazi na kufanya biashara kwa kufuata kanuni.Akizungumzia
kuhusu madai ya kuwapo kwa hali kuwa ngumu nchini Dr. Mengi pia
amewataka Watanzania kuichukulia hali hiyo kama fursa ya kubuni biashara
itakayowawezesha kupata faida kubwa.
Akiutambulisha
Mtandao wa Tanzania Venture Capital kwa wadau, Muasisi wake Bw. Salum
Awadh amesema Mtandao huo ni fursa kwa wawekezaji nchini kujipatia
mitaji ya kuanzisha ama kuendeleza biashara zao kwa ubia kwa masharti
rahisi.Alisema
kwamba wakati umefika kwa Tanzania kusonga mbele kutumia fursa zilizopo
duniani za mitaji na kusema jirani zetu wa Kenya wamesonga mbele katika
hilo.
Alisema
kwamba kutokana na kutojua umuhimu na ushiriki katika mitaji yenye
ubia, wananchi wengi wanakimbilia katika mabenki ya biashara ambako pia
wanapambana na vikwazo vingine.Alisema
kwa kuwa na kampuni ya mitaji inayoweza kutafuta pia mtaji
inayomilikiwa na wananchi wenyewe kupitia mitaji yao kutawezesha kuwapo
na uimara wa viwanda na kuongeza idadi zake kwa kuwa mfumo wa fedha wa
mitaji ni tofauti na kwenda benki.
Tanzania
kwa sasa ina zaidi ya mabenki 50 ambayo yanajishughulisha na mambo
mbalimbali yanayogusa biashara na hifadhi ya kawiada.Alisema
mazingira ya sasa yanahitaji mfumo mwingine wa ziada kusaidia
upatikanaji wa mitaji nje ya mabenki na kuzinduliwa kwa mtandao wa ubia
wa mitaji kutasaidia kuziba pengo lililopo.
Kwa
sasa Tanzania kwa rekodi zilizopo inapata asilimia 17 ya mitaji ya ubia
ya dola bilioni 2.4 iliyopo duniani huku Kenya ikiwa na nfasi nzuri
zaidi.Hafla
hiyo imehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi
nchini-TPSF Bw. Godfrey Simbeye, baadhi ya viongozi wa taasisi za
serikali na wafanyabiashara mbalimbali.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (kushoto),
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora (katikati)
pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Bw.
Godfrey Simbeye (kulia) wakiwasili kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania –
Tanzania Venture Capital Network uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye
(kushoto) akifafanua jambo kabla ya kuanza kwa uzinduzi wa Mtandao wa
Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network uliofanyika
katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Wanaomsikiliza ni Muasisi
wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh (wa pili kushoto
aliyesimama), Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr
Reginald Mengi (wa pili kulia) pamoja Mkurugenzi wa Uwekezaji na
Maendeleo ya Viwanda –TPSF, Edward Furaha (kulia).
Muasisi
wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh akitoa maelezo
kuhusu Mtandao wa Tanzania Venture Capital kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora (kushoto) kabla ya kuelekea
kwenye hafla ya uzinduzi wa mtandao huo iliyofanyika katika Hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Sekta Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye (wa pili kushoto) pamoja na
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi
(kulia).
Muasisi
wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh akitoa neno la
ukaribisho na kutambulisha mtandao huo ambapo amesema ni fursa kwa
wawekezaji nchini kujipatia mitaji ya kuanzisha ama kuendeleza biashara
zao kwa ubia kwa masharti rahisi wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa
mtandao huo ilyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi akitoa neno
la ufunguzi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora kutoa hotuba ya uzinduzi wa Mtandao
wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akitoa
hotuba ya uzinduzi rasmi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital ambapo
amesema umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo
katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda katika hafla
fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda –TPSF, Bw. Edward Furaha na
Aliyekuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Abdullah Mwinyi
wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye hafla ya
uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa
Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam.
Pichani
juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr.
Reginald Mengi akisalimiana na kubadilishana mawazo na wageni waalikwa
waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa wa Mtandao wa Tanzania Venture
Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi
akibadilisha na mawazo na Afisa Mtendaji Mkuu wa DOB Equity, Brigit van
Dijk-van de Reijt wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa Mtandao wa Tanzania
Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam. Wengine ni Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof.
Faustine Kamuzora (wa tatu kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya sekta Binafsi nchini-TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kushoto).
Tanzania
Venture Capital Network-TVCN katika picha ya pamoja na mdau
aliyewezesha kufanyika kwa uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture
Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment