Mwenyekiti wa Taasisi wa MO Dewji, Mohammed Dewji
Na Modewjiblog team
Mwenyekiti wa Taasisi wa MO Dewji,
 Mohammed Dewji kwa kushirikiana na kampuni ya Darecha Limited leo 
(jumatatu) wamezindua shindano la Mo Mjasiriamali lenye lengo la 
kusaidia kukuza ujasiriamali miongoni mwa vijana.
Shindano
 ya Mo Mjasiriamali litatoa fursa ya ukuzaji wa mitaji, ulezi wa 
wajasiriamali na mitandao ya biashara kuongeza mwanga, ujasiri na 
kuzalisha wajasiriamali Tanzania.“Mimi
 kama Mjasiriamali kijana na mzaliwa wa Singida vijijini, sikufikiria 
hata mara moja kama leo ningekuwa Mkurugenzi Mtendaji  wa moja ya 
makampuni yaliyofanikiwa sana katika nchi yetu na hata barani Afrika.” 
Inasema taarifa Mkurugenzi Mtendaji huyo wa MeTL kwa vyombo vya habari 
mwishoni mwa wiki.
Aidha
 alisema Afrika ni moja ya bara linalokua kwa haraka na lenye ukuaji 
imara wa uchumi na amini vijana wa Tanzania wana nafasi kubwa  ya 
kutumia fursa hizo ili kujiletea uchumi endelevu.
Lakini
 pamoja na ukweli huo changamoto kama za ukosefu wa mitaji, ukuzaji 
ujasiriamali na mitandao ya biashara zimekatisha tamaa vijana wengi 
kukuza kwa mafanikio makampuni yao hapa Tanzania na hivyo  kupunguza 
kasi ya ukuaji wa uchumi kwa watu wa kipato cha kati.
Kwa
 mujibu wa takwimu zilizotolewa na Benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), 
watu wenye kipato cha kati katika bara la Afrika wataongezeka na kufikia
 watu bilioni 1.1 ifikapo mwaka 2060.
Watu wa kipato cha kati ndio wanaochagiza ukuaji wa uchumi kutokana na mahitaji yao na pia ari ya ujasirimali.Pamoja
 na ukweli huo kunachangamoto nyingi zinawakabili watu hao wa kipato cha
 kati. Mathalani nchini Tanzania changamoto kubwa kwa vijana 
wajasirimali  ni gharama za kutafuta mtaji kwa kazi hizo.
“Kuna
 haja kubwa ya  kuhakikisha kwamba vijana hawa wanaondolewa tatizo la 
ujasirimali ili waweze kusukuma mbele uchumi wa Tanzania.” inafafanua 
taarifa hiyo.
Aidha
 kwa kuwa Tanzania inaelezwa kuwa ni nchi ya 19 katika bara la Afrika 
kuhusiana na fursa na ujasirimali ipo haja ya kusaidia ili kuiondoa 
katika nafasi hiyo. Taarifa ya nafasi ya Tanzania imo katika ripoti yake
 ya mwaka 2014 ya Africa Prosperity Report.
Taarifa ilifafanua zaidi kwamba kutokana na haja hiyo  Taasisi ya Mo Dewji na Darecha Limited wameungana pamoja na kuanzisha  shindano la Mo Entrepreneurs
 ili kutambua na kuuenzi mchango wa wajasirimali chipukizi na kufanikisha ndoto zao.
Ili
 kufanikisha nia ya kuwa na wajasiriamali wengi, shindano hilo 
linatarajiwa kuwa daraja kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji, Mohammed Dewji 
(MeTL Group na Mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation)
 ambapo vijana ambao wanaonekana wana kitu cha kufanya, lakini hawana 
msaada watashiriki kwa lengo la kupata msaada katika mfumo wa mtaji, 
mtandao na usimamizi wa ukuaji wa shughuli wanayofanya au kutaka 
kuifanya  ili kuianzisha na kuikuza.
Mambo
 hayo yatatekelezwa katika mfumo wa shindano litakalogusa wajasiriamali 
ambao  wana ari na nia ya dhati ya kuendeleza shughuli walizofikiria na 
kuzianzisha kwa lengo la kuinua uchumi wao binafsi na wa taifa.
Washindi
 watatu watakaotangazwa Aprili mwaka huu watapatiwa mtaji wa kuanzia au 
kuendeleza, pia watapatiwa maarifa ya kuendeleza shughuli zao na 
kuanzishwa mtandao wa kibiashara na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa MeTL 
Group  na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Mohammed Dewji.
Wakati
 akipewa tuzo ya Forbes ya mwaka 2015, Mohammed Dewji aliitoa  kwa 
heshima ya vijana akiwatakia kila la heri waking’aa, kuvunja nira ya 
woga, kukabili changamoto na kuendelea katika ujasiriamali kwa lengo la 
kufanya dunia yetu mahali bora pa kuishi.
Kwa habari zaidi tembelea: http://www.modewjifoundation.org/mo-entrepreneurs-competition
  SHARE 
  








No comments:
Post a Comment