TRA

TRA

Tuesday, May 3, 2016

KUELEKEA MIAKA KUMI YA MJENGWABLOG..

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Misimamo Mikali Ya Vijana Wa Mlimani (1)
- Julius Nyerere Alikoshwa Na Michango Ya Vijana Wasomi Wa Enzi Hizo..
Mwandishi Born Again Pagan ( BAP) Anaandika...
Makala haya kwanza yaliandikwa kwenye “Kijiji” chetu (mjengwablogspot.com) mwezi Mei, 2007, chini ya kichwa cha habari, “BAP Anavyomwelezea Yoweri Museveni”. Madhumuni yake
yalikidhi ombi la “Mwenyekiti wa Kijiji” kunitaka nitoe maelezo kidogo juu ya wanafunzi wenzangu Darasa la 1970 hapo Mlimani: Yoweri Kaguta Museveni na Hirji.
Nilianza kwa kutoa hoja kwamba haiwezekani kabisa kuweza kusimulia ya Yoweri Kaguta Museveni na Hirji bila kutoa, pengine, “background” ya miaka kumi ya kuanzia 1960 na jinsi matukio hayo yalivyojenga mikitadha iliyozalisha wanafunzi wenye msimamo mkali, kama akina Yoweri Kaguta Museveni na Hirji.
Katika makala haya yaliyohaririwa na kuongezea maelezo zaidi (pamoja na kubadili kichwa chake), ninagusia baadhi ya matukio ya miaka hiyo, na jinsi yaliyochangia katika kuivisha maisha ya ujana wa akina Yoweri Kaguta Museveni (Uganda), Hirji, Issa Shivji (Tanzania) pamoja na wengineo wengi waliomaliza hapo Mlimani mwaka 1970, kwa mfano:
Souma (Guinea), Archibord Kapote Mwakasungura (Malawi), John Garang (marehemu) wa Sudani, Salim Msoma, Issa Shivji, Nimrod Mkono, Moses Maira (marehemu), Ali Mchumo, James Kateka, Augustine Mahiga, Adamu Marwa, Pius Ngw’andu, Crispin Hauli, (marehemu), Abdallah Ngororo (marehemu), Patrick Qorro, Jenerali Ulimwengu, na wengine wengi sana,kama mimi.
Vile vile, makala haya yanachangia juu ya hali hapo Mlimani miaka yetu ya 1966-1970; mkwaruzano baina ya vyama vya wanafunzi vya USARF/TYL na USU kuhusu suala la “Rag Day”; umoja wa USARF na TYL; makala yanamtoa Hirji kando kidogo na kuzingatia tu ya Yoweri Kaguta Museveni (kwa makusudi); na mwisho, mgomo wa Jumamosi, 22 Oktoba, 1966.
Sisemi kuwa hao waliomaliza mwaka 1970 hapo Mlimani ndio tu maisha yao ya ujana yaliiva na kuwa na msimamo mkali. La hasha! Wengine walikuwa hawana msimamo huo! Na walikuwepowengine nyuma yetu wenye msimamo mkali, pia, ikiwa ni pamoja na hao waliotutangulia. Ila nawataja hao wa mwaka 1970 kwa sababu ndio lilikuwa darasa letu.
Matukio ya Miaka Kumi Kuanzia 1960
Tumetoka mbali; tunakwenda mbali, pia. Kati yetu (wewe na mimi) huko tuendako hakuna aliyewahi kupafikia, ingawa tunapanga kuwasili huko. Miaka kumi ya kuanzia 1960 ilikuwa yamatukio mengi na mikakati mingi, ki-ulimwengu na ki-taifa (Tanzania). Ufuatao ni mtiririko wa matukio na mikakati hiyo; lakini si ki-miaka (chronology).
Moja, misukosuko ya ki-mataifa ya miaka ya kuanzia 1960 ilikuwa ni kupanuka kwa itikadi eti ya u-Komunisti. Kudhibiti kupanuka kwa u-Komunisti duniani kuliongozwa na Amerika ikisaidiana na Nchi za Magharibi, mithili ya hadithi ya kuweka kifuniko jini lisitoke kabisandani ya chupa!
Nchi hizi ziliuona u-Komunisti kuwa ni utamaduni uliowania kuua ule wa ki-Bepari. Michakatohiyo ikazua, eti, Vita Baridi! Amerika ilikania kudhibiti (to contain) kupanuka kwa u-Komunisti huko Asia ya Mashariki ya Mbali, Amerika ikawania kuishambulia Vietnam.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger