Meneja wa
Kanda Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) Kanda ya Nyanda za
Juu Kusini Ndugu Hiraly Maskini akifungua Mkutano wa wadau wa soko la
Bima kutoka Mikoani ya Nyanda za Juu Kusini (hawapo pichani) katika
ukumbi wa Mikutano Mkapa jijini Mbeya Mei 3 -2016 mkutano ambao unalengo
la kujadili na kutambua changamoto mbalimbali wanazo kutana nazo wadau
hao katika kutekeleza majukumu yao.(Picha Emanuel Madafa,Jamiimojablogu-Mbeya)
Wadau wa
soko la Bima Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juuu
Kusini,Mbeya,Iringa,Njombe ,Rukwa ,Songwe na Katavi wakiwa katika
umakini kufuatilia agenda mbalimbali katika mkutano huo ulioandaliwa na
Mamlaka ya usimamizi wa Bima Nchini Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
(TIRA).
Kaimu
Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)Mkoa wa Mbeya Ndugu Victory
Mleleu akichangia moja ya maada katika mkutano huo ulihusisha wadau wa
soko la Bima Kanda ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na Mamlaka ya
usimamizi wa Bima (TIRA) semina ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Mkapa
jijini Mbeya Mei 3 mwaka huu.
Mhasibu
wa Kanda Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini Ndugu Kurenje Mbura akiwasilisha moja ya maada katika mkutano wa
wadau wa Soko la Bima ulioitishwa na Mamlaka hiyo ya (TIRA ) Mei 3 Mwaka
huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya.
Mmoja wa
wadau wa soko la Bima Mkoani Mbeya Ndugu Masterdy Luvanda akichangia
maada katika mkutano wa wadau wa Soko la Bima ulioitishwa na Mamlaka ya
Usimamizi wa Bima (TIRA) katika Ukumbi wa Mkapa jinini Mbeya Mei 3
mwaka huu, ukiwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali wanazo
kutanana nazo wadau hao sanjali na kupeana uzoefu katika sekta hiyo.
Picha ya Pamoja Meza kuu na washiriki wa semina hiyo.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment