TRA

TRA

Sunday, May 8, 2016

Makamu wa Rais Samia kapiga STOP kodi zote za biashara zinazowadhalilisha wanawake

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Mei 8 2016 ni siku ya wakinamama Duniani, Tanzania pia imekuwa moja ya nchi iliyofanya maadhimisho hayo, Hapa nakukutanisha na Makamu wa Rais Samia Suluhu ambaye leo alikuwa Dodoma na baada ya kuhutubia wananchi wake akaguswa na hili la kodi kwa wafanyabiashara wanawake na kutoa maamuzi..
Mimi kama mama nachukizwa na jambo moja kubwa nililoliona kule Moshi na baaadhi ya maeneo kule Arusha, kuna kodi zinatolewa katika masoko, Ukipita masoko ya Moshi na Arusha Unakuta wakinamama wanasimama na ndizi kichwani anasimama na ndizi yake hadi aiuze’
‘Na akiiweka chini anatozwa kodi na kodi ile ni sawa na bei anayoiuza. Kwahiyo mama anabakia na ndizi yake kichwni mpaka aiuze.’
‘Naelekeza Wakurugenzi wa halmashauri kufuta kodi hiyo mara moja, na nitafanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa jambo hili. Na siotu kodi za ndizi bali kodi zote zinazowazalilissha wakinamama’
_MG_0067
Wakinamama wa Dodoma kwenye maadhimisho
_MG_0072
_MG_0163
Makamu wa Rais Samia Suluhu akipewa zawadi ya Picha

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger