TRA

TRA

Wednesday, May 11, 2016

Mameya wa zamani Rwanda washtakiwa Ufaransa

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


 
Symbolbild - Ruanda Opfer des Bürgerkriegs
Mameya wawili wa zamani wa nchini Rwanda lwanapandishwa kizimbani katika mahakama nchini Ufaransa kwa shutuma za makosa ya kibinadamu na kushiriki mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Octavian Ngenzi na mwenzake Tito Barahira kwa pamoja wanatuhumiwa kuwa na mchango wa moja kwa moja katika mauaji hayo.
Kesi hii ya pili kufunguliwa na mahakama maalum iliyoundwa na Ufaransa kwa ajili ya kuwashitaki watuhumiwa wa Kinyarwanda waliokimbilia nchini humo, inatarajiwa kubainisha mwelekeo wa mahusiano baina ya nchi hizo mbili.
Kwa miongo miwili sasa, Rwanda imekuwa ikiituhumu Ufaransa kwa ushiriki katika mauaji ambayo yaliwaua raia laki nane, ikisema kuwa Ufaransa iliisaidia serikali ya wakati huo iliyokuwa ya Kihutu. Miaka miwili baadaye katika kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji hayo, rais wa nchi hiyo Paul Kagame aliwatuhumu waziwazi wanajeshi wa Ufaransa sio tu kwa kusaidia bali kwamba walihusika moja kwa moja katika mauaji hayo.
Na sasa Octavian Ngenzi na Tito Barahira wanapandishwa kizimbani kwa ushiriki wao wa moja kwa moja wa kuwaua mamia ya wakimbizi wa Kitutsi waliokuwa wamejihifadhi katika kanisa mnamo aprili 13 mwaka 1994 huko mashariki mwa mji wa Kabarondo.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger