
Nigeria imeshangazwa na kusikitishwa na kauli iliyotolewa na waziri mkuu wa Uingereza kwamba nchi hiyo inaongoza kwa rushwa.
David Cameron aliitaja Nigeria na Afghanistan kuwa ni nchi mbili duniani zinazoongoza kwa rushwa na ufisadi.
Ingawa
kauli hiyo hakuitoa rasmi kwa vyombo vya habari, lakini Bwana Cameron
ameonekana katika kamera akiwa ndani ya kasri ya Buckingham akimwambia
malkia Elizabeth kwamba viongozi wa baadhi ya nchi ambazo zinaongoza kwa
ufisadi duniani watahudhuria mkutano dhidi ya ufisadi unaotarajiwa
kuanza hapo kesho chini ya uwenyeji wa David Cameron.
Garba
Shehu msemaji wa Rais Muhammadu Buhari anasema wameshangazwa na
kuhuzunishwa na kauli hiyo kwa sababu imeshindwa kuzingatia kwazi kubwa
inayofanywa na rais Buhari kuondoa rushwa serikali.
''
Tunaamini kwamba waziri mkuu alikua akiangalia picha ya zamani ya
Nigeria, ambayo tayari imeondolewa, dunia nzima inaangalia mapambano
yanayofanyika dhidi ya rushwa, na tunaamini ni kutokana na mafanikio
hayo ndio Rais Buhari amealikwa sio tu kama mgeni bali miongoni mwa
watakaotoa mada." alisema.
Agenda
kuu iliyomwingiza madarakani Rais Buhari ni ile ya kutokomeza rushwa na
kupambana na kundi la Boko Haram na kuhakikisha kuwa wanafunzi wa kike
waliotekwa na kundi hilo, wanapatikana. Hata hivyo, kadri siku
zinavyokwenda, ndiv
SHARE








No comments:
Post a Comment