TRA

TRA

Sunday, May 8, 2016

MTANGAZAJI WA CNN RICHARD QUEST AFURAHISHWA NA VIVUTIO VUA UTALII TANZANIA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


A4
Kwa mara nyingine tena Tanzania inashiriki katika onesho la kimataifa la Utalii la INDABA yanayofanyika huko Afrika Kusini maonesho hayo yalianza  jana  tarehe 7 Mei na  yanatarajiwa kumalizika tarehe  9 Mei, 2016.  jijini Durdan, Bodi ya Utalii (TTB) ndio waratibu wa onesho kwa upande wa Tanzania. Katika onesho hili TTB inashirki pamoja na taasisi za TANAPA na Mamlaka na Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na makampuni mbalimbali binafsi Zaidi ya 30 ya sekta ya Utalii .
Katika siku yake ya kwanza Banda la Tanzania limetembelewa na wadau wengi wakiwemo watalii, waandishi wa habari za utalii, mawakala wa Utalii nk. Miongoni mwa watu mashuhuri waliotembelea Banda la Tanzania ni Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest ambaye alifurahishwa na vivutio vua utalii nchini Tanzania mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Maofisa wa Bodi ya Utalii  Tanzania TTB.
A05
Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimuonyesha jambo Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini..
A3
Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimpa maelezo kuhusu vivutio vya utalii nchini Tanzania  Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini Katikati ni Bi Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger