BABA
Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati)
akiwa na Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael
Kagondela kulia na Mhasibu wa mtandao huo, Asha Salvador baada ya
kumkabidhi kadi ya uanachama na katiba baada ya kikao cha kuthibitisha
mwanae kukubali kupewa ekari tano za kujenga kituo cha wanamichezo,
Mkuranga
BABA
Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati)
akijaza fomu za kukubali masharti ya kujiunga na Mtandao wa Wasanii
Tanzania (SHIWATA) mbele ya Mhasibu wa mtandao huo Asha Salvador.
Na Mwandishi Wetu
MTANDAO
wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa sherehe za kumkabidhi eneo la
kujenga kituo cha michezo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta katika
sherehe zitakazofanyika Juni 4, 2016 kwenye kijiji cha Wasani Mwanzega
Mkuranga.
Mwenyekiti
wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa maandalizi ya
sherehe hizo itaambatana na ugawaji nyumba 31 kati ya hizo moja kubwa,
tatu ndogo na misingi 27 ya nyumba hivyo kufikisha jumla ya nyumba 150.
Alisema
baba yake Mbwana Mzee Ali Samatta amethibitisha kuwepo kwa mwanae katika
sherehe hizo ambazo naye ametunukiwa kuwa mwanachama wa heshima wa
mtandao huo na kukubali kushirikiana kuhakikisha michezo inakuwa nchini.
“Baba
yake Samatt alisema wakati akiwa kijana alikuwa mfungaji mzuri kwa timu
alizowahi kuchezea miaka ya sitini kama vile timu ya shele ya Sekondari
ya Mzumbe, timu ya mkoa wa Morogoro, timu ya Polisi na badaye aliwahi
kuichezea Simba akiwa na akina Hamisi Kilomoni” alisema Taalib.
Alisema
sherehe hizo pia zitapambwa na wasani kutoka vikundi mbalimbali vya
ngoma na sarakasi kutoka jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani..
Alisema
SHIWATA ilimzawadia uanachama wa heshima mchezaji huyio baada ya
kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika na kutangaza kumpatia eneo la
ekari tano kwa ajili ya kujenga kituo cha wanamichezo.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment