Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza
Yussuf Manji kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Young Africans SC
baada ya kupata kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa. Kura mbili
ziliharibika kwa nafasi hiyo.
Kadhalika
Rais Jamal Malinzi amempongeza Clement Sanga kwa kuchaguliwa kuwa
Makamu Mwenyekiti baada ya kupata kura 1,428 wakati mpinzani wake Titus
Osoro alipata kura 80. Kura 1,508 zilipigwa katika nafasi ya kuwania
makamu mwenyekiti.
Kadhalika
wajumbe wanane wanaounda Kamati ya Utendaji kwa kuchaguliwa kuongoza
Klabu ya Young Africans kwa miaka minne ijayo kwa mujibu wa katiba.
Wajumbe
waliochaguliwa ni Omary Said (1,069), Siza Lyimo (1,027), Salum Mkemi
(894), Thobius Lingalangala (889), Ayoub Nyenzi ((889), Samwel Lukumay
(818), Hussein Nyika (770) na Hashim Abdallah (727.
Katika
salamu hizo za pongezi, Rais Jamal Malinzi pia amewapongeza wanachama wa
Young Africans kwa kufanya uchaguzi wa amani na utulivu.
Kutokana
na hali hiyo, Rais Jamal Malinzi amewataka uongozi huo wa Young Africans
kufungua ukurasa mpya wa kuendesha klabu hiyo na kuiletea mafanikio
klabu hiyo kongwe na maarufu katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki
na Kati hasa wakati huu ambako Young Africans inashiriki hatua ya
makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment