Vikosi
vinavyounga mkono serikali ya Umoja wa kitaifa ya Libya vikiingia katika
mji wa Sirte , ngome ya Islamic State 09 Juni 2016
Majeshi
yanayo shirikiana na serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya jana Jumamosi
yamesema yamefanikiwa kurejesha mikononi mwao mji wa bandari wa Sirte
uliokuwa mikononi mwa udhibiti wa kundi la Islamic State.
Kudhibitiwa
kwa mji wa Sirte, alikozaliwa Moamer Kadhafi itakuwa pigo kubwa kwa
wapiganaji hao wenye msimamo mkali ambao pia wamepoteza maeneo kadhaa
nchini Syria na Iraq ambayo walijitangazia kuwa ya Kiislamu.
Vikosi
vya Libya pia vimerejesha maeneo ya makazi mashariki mwa Sirte, ambayo
kwa mwaka uliopita yamekuwa ngome kuu za kundi la Islamic State katika
nchi za Afrika Kaskazini, msemaji wa majeshi, Rida Issa, ameiambia AFP.
Wanajihadi
kwa sasa wamezungukwa katika eneo la kilomita za mraba zipatazo tano
ndani ya mji wa Sirte ambako wameweka mitego yao ya mabomu isiyo na
madhara asema msemaji wa majeshi.
Aidha Issa ameongeza kuwa wakkazi wengi wa mji huo wame kimbia lakini baadhi yao wapatao elfu thelathini wamebaki.
Mjumbe wa
Umoja wa Mataifa nchini Libya Martin Kobler jana Jumamosi ameandika
katika ukurasa wake wa Twitter kuwa amefurahishwa na hatua za haraka
zilizopigwa na majeshi yanayounga mkono serikali ya Umoja wa Kitaifa ya
Libya.
Ufaransa
pia imepongeza hatua hiyo na kutoa wito kwa pande zinazohasimiana
kisiasa nchini Libya kuungana dhidi ya kundi la Islamic State.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment