Mbele ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya, baada ya shambulio la afisa wa polisi kwa kisu, Oktoba 27, 2016.
Marekani
imeamua kufunga kwa muda Ijumaa hii ubalozi wake nchini Kenya kufuatia
kisa cha kijana mmoja kupigwa risasi Alhamisi hii Oktoba 27 alasiri
mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, baada ya kujaribu kumchoma
kisu polisi wa Kenya ambaye alikua akitoa ulinzi kwenye eneo
kunakopatikana ubalozi huo.
Uchunguzi umeanzishwa, lakini hakuna dalili yoyote inayoonyesha kama ilikua shambulizi la kigaidi.
Polisi
aliyekuwa amelengwa ni kutoka kikosi chacha kijeshi cha polisi wa Kenya
(GSU), wanaohusika na kutoa ulinzi katika eneo lililo karibu na ubalozi
wa Marekani.
"Ni mpita
njia ambaye alikuwa akitembea katika mtaa wa Umoja wa Mataifa,
alimshambulia kwa kisu mmoja wa askari polisi, alimchoma kisu kichwani,
amesema Vitalis Otieno, mkuu wa polisi wa eneo la Gigiri. Polisi huyo
alijihami kwa kumpiga risasi mtu huyo na kufaulu kumuua. "
Afisa huyo aliyejeruhiwa alipelekwa mara moja hospitalini ambapo anaendelea vizuri kwa mujibu wa viongozi.
Mashahidi
katika eneo la tukio wamesema kwamba mshambuliaji anayeonekana kutoka
kabila la Somalia, alimshambulia polisi kwa kisu. Mfanyakazi wa mgahawa
uliyo karibu na eneo la tukio ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema
kuwa aliona polisi akimpiga risasi mtu mmoja ambaye alikua na kisu
mkononi baada ya kudondoka.
Kijana
huyo ana umri wa miaka 24 na ni kutoka kaunti ya Wajir inayopakana na
Somalia, polisi imesema, huku ikikataa kutoa maelezo zaidi kuhusu chanzo
cha tukio hilo Wakati huo huo . RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment