Kocha
Mkuu wa klabu ya Sunderland ya Uingereza David Moyes ameshtakiwa na
chama cha soka cha Uingereza kwa utovu wa nidhamu wakati wa mechi dhidi
ya Southampton Jumatano.
Southampton
walishinda mechi hiyo ya Kombe EFL Cup uwanjani St Mary’s kupitia bao
la Sofiane Boufal na kuwafanya vijana wa Moyes kuyaaga mashindano hayo
ambayo yamefikia katika hatua ya robo fainali.
Chama cha
Soka cha Uingereza (FA) kimesema kuwa ,Moyes alitumia lugha ya kutusi
au maneno ya kuudhi akiyaelekeza kwa mwamuzi wa mechi baada ya timu yake
kufungwa.
Kisa
hicho kilitokea dakika ya 90 refa Chris Kavanagh alipokataa kuwapa
Sunderland penalti baada ya mshambuliaji wa Sunderland Victor Anichebe
kuonekana kuchezewa visivyo eneo la hatari na beki wa Southampton huku
zikiwa dakika za majeruhi.
Moyes,
aliyeteuliwa kuwa Kocha wa Sunderland wanaojulikana kuwa Paka Weusi
Julai, ameshinda alama mbili pekee kutoka kwa mechi tisa ligini na
wakiwa na kibarua kingumu watakapowaalika washika bunduki Arsenal hapo
kesho.
Aidha kwa
mujibu wa FA imempa kocha huyu uhuru wa kujieleza na kujitetea hadi saa
tisa alasiri kwa saa za Afrika Mashariki Jumanne kujibu tuhuma hizo. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment