Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kushoto)
akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama, Taarifa ya Tathmini
Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 kwenye
ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mst. Damian Lubuva (kushoto) na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu Mhe. Jenista Mhagama, wakionesha Taarifa ya Tathmini Baada ya
Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 ambayo ilikabidhiwa
kwa Mhe. Waziri na NEC kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu
Mhe. Jenista Mhagama akihutubia kwenye mkutano wa kukabidhiwa Taarifa ya
Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015,
kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma
.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mst.
Damian Lubuva na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mst. wa Zanzibar
Hamid Mahmoud Hamid..
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mst. Damian Lubuva akitoa
maelezo kuhusu Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na
Madiwani wa Mwaka 2015 ambayo aliikabidhi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista
Mhagama kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini
Dodoma .
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani
akitoa maelezo ya Utangulizi kuhusu Taarifa ya Tathmini Baada ya
Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015, ambayo Tume
iliikabidhi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,
Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) kwenye ukumbi
wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma jana.Katikati
ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mst. wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid.
Baadhi ya
washiriki wa mkutano wa makabidhiano ya Taarifa ya Tathmini Baada ya
Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 wakifuatilia hotuba
ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva
(aliyesimama mbele).Taarifa hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista
Mhagama, kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni
mjini Dodoma jana. Picha zote na Hussein Makame-NEC, Dodoma
Christina Njovu-NEC, Dodoma
Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekabidhi Taarifa ya Tathmini baada ya Uchaguzi
wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu , Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Walemavu Mh. Jenista
Mhagama mjini Dodoma jana.
Akikabidhi
taarifa hiyo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damin
Lubuva alisema kuwa Tathmini hiyo imeonesha kuwa Tume hiyo imefanikiwa
kwa kiasi kikubwa kuendesha na kusimamia uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge
na Madiwani uliofanyika Oktoba 25 mwaka 2015.
Alisema
kwa mujibu wa tathmni hiyo Tume imebaini kuwa sheria, kanuni na
zilizotumika wakati wa Uchaguzi mkuu zilikuwa chachu ya kufanikisha
Uchaguzi Mkuu, Watendaji wa Uchaguzi walionesha kuwa na uelewa wa
kutosha wa Shriea na Kanuni za Uchaguzi.
Jaji Mst.
Lubvuva alisema kuwa lengo la tathmini hiyo ni kupata taswira halisi ya
Tume kutoka kwa Wadau kwa lengo la kujenga msingi bora wa utekelezaji
wa chaguzi zijazo na kujua kwa nini baadhi ya maeneo yalikuwa na
mwitikio mdogo katika kupiga kura wakati yalikuwa na mwitikio mkubwa
kwenye kuandikisha wapiga kura kwenye Daftari la kudumu la Wapiga Kura.
Alisema
kuwa Tathmini hiyo ni ya kwanza kufanyika tangu kuanzishwa kwa Tume hiyo
mwaka 1993 ambayo imeweza kuwapatia mrejesho juu ya utekelezaji wa
Uchaguzi Mkuu kutoka kwa wadau wa Uchaguzi .
Alibainisha
kuwa wakati wa tathmini hiyo wadau wengi walionesha kuridhishwa na
utendaji wa Tume katika kusimamia Uchaguzi Mkuu na kutangaza matokeo kwa
kufuata sheria na kanuni zilizopo.
Akipokea
Taarifa hiyo , Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuweza kufanikisha Uchaguzi Mkuu ulikuwa
na changamoto nyingi na ushindani mkubwa wa kisiasa na kufanikiwa
kufanya tathmini ya Uchaguzi Mkuu ambayo imekabidhia kwake kwa niaba ya
Serikali.
“Ni kweli
kwamba wananchi wengi wamekuwa na mwamko wa kisiasa katika jamii yetu,
hasa vijana , hivyo taarifa hii itasaidia sana wananchi kuifahamu vyema
zaidi namna Tume inavyosimamia , kuendesha na kuratibu mchakato mzima wa
Uchaguzi kuanzia uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, hadi
kutangaza matokeo.” Alisema Waziri Mhagama.
Alisema
Tathmini hii itawawezesha wadau mbalimbali kuitumia kama nyenzo muhimu
katika kushiriki na kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo.
Naye
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Bw. Ramadhan Kailima katika maelezo ya
utangulizi alieleza kuwa tathimini hiyo ilitumia njia ya mahojiano ya
ana kwa ana na majadiliano na ilijumuisha makundi 192 ya wazee wenye
umri wa zaidi ya miaka 60 na makundi 192 ya vijana wenye umri kati ya
miaka 18 na 35.
Alisema
matokeo ya tathmini hiyo yanaonesha kuwa kati ya watendaji 1,029
walihojiwa na watendaji wengi kati wao walisema taratibu mbalimbali za
uchaguzi hadi kutangaza matokeo zilizingatiwa.
Bw.
Kailima aliongeza kuwa kuhusu Elimu ya Mpiga Kura wadau wa Uchaguzi
1,915 waliohojiwa kuhusu uelewa wao juu ya Elimu ya Mpiga Kura kati yao
Wadau 1,463 sawa na asilimia 76.4 walisema kuwa walikuwa na uelewa wa
Elimu ya Mpiga Kura na Watu 452 sawa na asilimia 23.6 hawakuwa na
uelewa.
Kutokana
na tathmini hiyo Bw. Kailima alisema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
imejipanga kutoa Elimu ya MpigaKura kwa lengo la kuwafikia wananchi na
wadau moja kwa moja na imeweza kushiriki katika maonyesho mbalimbali
yakiwemo ya Sabasaba, Nanenane , Mkutano wa Tawala za Mitaa Tanzania na
Wiki ya Vijana iliyofanyika Mkoani Simiyu.
Sambamba
na hilo, aliongeza kuwa Tume imepanga kuhudhuria na kutoa Elimu katika
mikutano ya viongozi mbalimbali ikwemo viongozi wa Dini, Mabaraza ya
Madiwani na mikutano mikuu ya vijiji na mitaa.
Kutoa
elimu ya Mpiga Kura kwa njia ya luninga, redio, mabango na mitandao ya
kijamii, Kutoa vibali vya kutoa elimu ya Mpiga kura kwa Taasisi na
Asasi.
Kufanyika
kwa tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka
2015 ni mojawapo ya ukamilishaji wa mzunguko wa Uchaguzi huo ambao
ulitanguliwa na zoezi kukabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge
na Madiwani kwa Mh. Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu jiji
Dar es Salaam na ni mwanzo wa kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi mwingine. (P.T
SHARE
No comments:
Post a Comment