Wanajeshi watatu wamekamatwa nchini Sudan Kusini kwa tuhuma za
ubakaji. Msemaji wa kijeshi ameeleza kwamba tukio hilo lilitokea nje ya
mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba ambako viongozi wa kijamii waliripoti
kwamba wanawake wasiopungua 10 pamoja na mtoto mmoja walibakwa na
kuteswa. Hatua hii imetokana na ahadi ya rais Salva Kiir ya kuwafikisha
mbele ya sheria, wanajeshi waliofanya vitendo vya ubakaji na dhulma za
kingono dhidi ya raia. Inaaminika maelfu ya wanawake na wasichana
walibakwa nchini Sudan Kusini ambayo haina utulivu, baada ya kuzuka kwa
mgogoro wa kijeshi kati ya rais Kiir na makamu wake wa zamani Riek
Machar mnamo mwezi Desemba 2013.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment