Staa wa soka wa kimataifa wa Hispania anayeichezea Atletico Madrid, Fernando
Torres usiku wa March 2, 2017 alishtua mashabiki wa soka na wachezaji
wenzake kufuatia kupata jeraha kichwani na kufanya kila mchezaji aliyepo
uwanjani kushtuka na jeraha hilo.
Torres, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Atletico Madrid kilichocheza na Deportivo la Coruna katika
mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, alilazimika kukimbizwa
hospitali na ambulance kufuatia kuumia kichwani na kupoteza fahamu baada
ya kugongwa na Alex Bergantinos dakika ya 85.
![](https://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2017/03/14513781303301.jpg?zoom=1.100000023841858&resize=620%2C392)
Taarifa kutoka Hospitali ambayo staa huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea aliyezichezea timu hizo kwa nyakati mbili tofauti, amepata fahamu na Atletico wameripoti kuwa atakuwa katika uangalizi wa daktari kwa usiku wote huu.
SHARE
No comments:
Post a Comment