Wizara ya ulinzi ya Sweden jana imetangaza kurejesha mpango wa
utumishi wa laazima jeshini, mnamo wakati wasiwasi unaongezeka kuhusu
vitendo vya Urusi nchini Ukraine. Sweden iliufuta mpango huo mwaka 2010,
lakini mizozo ya kikanda imeilaazimu serikali kwa mara nyingine
kuandikisha vijana kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi. Uandikishaji
wanajeshi utaanza rasmi mwaka 2018, na utajumlisha watu waliozaliwa
mwaka 1999 au baada ya hapo, ambapo karibu watu 13,000 wametakiwa
kuripoti kwenye usaili, na 4000 watachaguliwa kwa ajili ya mafunzo.
Uandikishaji huo utahusisha wanawake, ambao tayari wanachangia hadi
asilimia 16 ya jeshi la Sweden lenye jumla ya watu 20,000.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment