Paa la hospitali moja ya umma nchini Afrika Kusini limeanguka na
kujeruhi watu kadhaa. Wagonjwa na wafanyakazi katika hospitali ya
Charlotte Mexeke mjini Johannesburg walikwama ndani ya jengo baada ya
paa lake kuporomoka wakati mafundi ujenzi wakijaribu kuziba sehemu
iliokuwa inavuja. Watu wasiopungua watano walipata majeraha, na
haikubainika mara moja wangapi walikuwa wamekwama katika jengo hilo.
Picha za TV zilionyesha waokoaji wakiondoa vifusi katika juhudi za
kuwafikia watu waliokwama ndani ya hospitali hiyo. Maafisa wamesema
tukio hilo linamulika tatizo la uhaba wa ufadhili unaoukabili mfumo wa
sekta ya afya ya umma nchini Afrika Kusini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment