Siku chache baada
ya wanasayansi kubaini mti mrefu zaidi barani Afrika katika Mlima wa
Kilimanjaro nchini Tanzania sasa wataalam hao wamefanya ugunduzi
mwengine kuhusu mti huo.
Wataalam hao kutoka chuo kikuu cha Beyreuth Ujerumani sasa wamegundua kwamba mti huo ndio ulio na miaka mingi zaidi duniani.Kulingana na gazeti la Mwananchi nchini Tanzania, Mtafiti wa viumbe hai na mazingira kutoka Chuo hicho Dk Andrew Hemp ameelezea sifa za mti huo ujulikanao kama Mkukusu kuwa unaweza kuishi kati ya miaka 200 hadi 300, lakini ulioonekana nchini una miaka 600.
Mti huo unapatikana katika Kijiji cha Tema wilayani Moshi, na upo katika eneo lililopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (kinapa).
Dk Andrew amesema kwa mujibu wa utafiti mti huo una uwezo wa kuishi miaka hiyo kwa kutunzwa na kuhifadhiwa.
- Mti mrefu zaidi Afrika wagunduliwa Tanzania
- Utamaduni wa kutoa majina Afrika: Njia tisa za kumpatia jina mtoto wako
Tayari Serikali imeiagiza Kinapa kuboresha miundombinu ya barabara ili kuweza kuufikia mti huo iwapo watalii watataka kwenda kuuona.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki amesema mti huo utasaidia kuongeza mapato kwa kasi kwa kuwa ni kivutio kipya cha utalii ndani ya mkoa huu.
Mhifadhi Mkuu wa Kinapa, Betrita Loibok amesema agizo hilo litazingatiwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) ili mti huo uweze kuwa kivutio ndani na nje ya chini
SHARE
No comments:
Post a Comment