NA K-VIS BLOG
BENKI Kuu ya Tanzania, (BoT), imeifutia leseni ya
kufanya shughuli za kibenki, Benki ya FBME Bank Limited, kuanzia leo Mei 8,
2017 na kuiweka chini ya ufilisi.
Taarifa ya Benki kuu iliyotolewa Mei 5, 2017 na
kusambazwa kwenye vyombo vya habari leo Mei 8, 2017 tayari imeteua Bodi ya Bima
ya Amana kama mfilisi kuanzia leo hii Mei 8, 2017.
Aidha taarifa hiyo imewataka wenye amana, wadai na
wadaiwa wawe wavumilivu wakati Mfilisi akiandaa utaratibu wa kushughulikia
stahiki zao
SHARE
No comments:
Post a Comment