TRA

TRA

Monday, May 8, 2017

Rais Muhammadu Buhari arejea London kwa matibabu

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amerejea London kupokea matibabu wiki chache baada yake kukaa huko kwa miezi miwili.
Taarifa kutoka kwa ikulu ya rais huyo imesema amehitajika kwenda Uingereza kuchunguzwa na madaktari.

 Buhari alijitokeza wakati wa swala ya Ijumaa msikitini katika ikulu wiki iliyopita 

Hata hivyo, kufikia sasa hakuna taarifa kuhusu ugonjwa anaougua wala muda ambao anatarajiwa kukaa nchini Uingereza.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema Jumapili ilikuwa siku muhimu kwa Muhammadu Buhari ambapo alikuwa anakutana na wasichana 82 wa Chibok ambao walikuwa wameachiwa huru baada ya kuzuiliwa na wanamgambo wa Boko Haram kwa miaka mitatu.
Badala yake, kutokana na afya yake, tukio hilo la kuwapokea halikufanywa kuwa sherehe kubwa.
Buhari amekuwa haonekani sana hadharani kipindi kirefu cha mwaka huu.
Alikaa wiki saba Uingereza kabla ya kurejea Machi.
Wiki iliyopita, hakuhudhuria mikutano mitatu ya baraza la mawaziri huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu hali yake.
Alijitokeza hata hivyo Ijumaa wakati wa swala ya Ijumaa katika msikiti ulio ikulu ya nchi hiyo.


 Buhari alipojitokeza katika ikulu Ijumaa 

Taarifa kutoka ikulu imesema kiongozi huyo alikuwa amepangiwa kuondoka mapema Jumapili alasiri lakini akachelewa kwa muda kumuwezesha kukutana na wasichana hao wa Chibok.

Haki miliki ya picha Nigeria presidency
Image caption Buhari alipojitokeza katika ikulu Ijumaa
Rais Buhari amesema: "Nina imani kwamba serikali itaendelea kutekeleza shughuli zake vyema nitakapokuwa nje ya nchi."

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger