Mkwe wa rais Donald
Trump na mshauri mkuu Jared Kushner anachunguzwa na shirika la FBI
ikiwa ni miongoni mwa uchunguzi wa Urusi kulingana na vyombo vya habari
nchini Marekani.
FBI linachunguza hatua ya Urusi kuingilia uchaguzi wa urais wa 2016 nchini humo na ushirikiano wa kundi la kampeni la rais Trump.
Rais Trump amekana madai yoyote ya kujihusisha na Urusi wakati wa kampeni.
Jared Kushner na mkewe Ivanka Trump
Wakili wa bwana Kushner amesema kuwa mteja wake atashirikiana na wachunguzi hao kuhusu uchunguzi wowote.
Rais Trump ametaja hali hiyo kuwa 'uwindaji' mkubwa wa kiongozi katika historia ya Marekani.
- FBI: Tunachunguza madai ya Urusi kuingilia uchaguzi Marekani
- FBI imethibitisha kuichunguza Urusi
- Trump: Sichunguzwi na FBI
- Trump amfuta kazi mkurugenzi wa FBI James Comey
- Putin aahidi kutoa siri za mkutano wa Trump
Maafisa wa Marekani waliotajwa waliambia chombo cha habari cha NBC kwamba hatua ya kumchunguza bwana Kushner mwenye umri wa miaka 36 haimaanishi kwamba wachunguzi wanamshuku kuhusu uhalifu fulani na kwamba wanataka kumshtaki.
Kwengine ,gazeti la Washington Post limeripoti kwamba wachunguzi hao walikuwa wakiangazia mikutano aliofanya mwaka uliopita na balozi wa Urusi nchini Marekani ,Sergei Kislyak na mfanyikazi mmoja wa benki kutoka Moscow.
Bunge la Congress pia linachunguza hatua hiyo ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani na ushirikiano wowote na rais Trump.
Bwana Kushner tayari amekubali kuzungumzia kuhusu uhusiano wake wa Urusi na kamati ya kijasusi ya bunge la seneti.
''Bwana Kushner hapo awali alijitolea kuzungumza kuhusu kile anachokijua kuhusu mikutano hiyo'', wakili wa Kushner, Jamie Gorelick aliambia BBC.
''Atafanya hivyo iwapo atahitajika kuhusiana na uchunguzi mwengine wowote'' ,aliongezea.
- Trump ''alitaka FBI kusitisha uchunguzi wa Flynn''
- Clinton: Nalaumu FBI na wadukuzi wa Urusi
- Trump amuonya mkuu wa FBI aliyefutwa James Comey
Ikulu ya Whitehouse imekumbwa na mizozo kufuatia madai kwamba rais Trump alimtaka aliyekuwa mkuu wa FBI kuwacha uchunguzi kuhusu uhusiano kati ya aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama Michael Flynn na Urusi.
Bwana Flynn alilazimishwa kujiuzulu mnamo mwezi Februari baada ya kumdanganya makamu wa rais kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi kabla ya rais Trump kuchukua mamlaka. Mnamo mwezi Januari.
Urusi mara kwa mara imekana kuhusishwa na uchaguzi wa urais nchini Marekani.
SHARE
No comments:
Post a Comment