Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi
wa michezo ya Umisseta Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini
Mbeya mwishoni mwa wiki.
Meneja
Masoko Msaidizi wa Coca-Cola,Pamela Lugenge,akiongea wakati wa hafla
ya uzinduzi wa michezo ya Umisseta Copa Coca Cola katika uwanja wa
Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu
za shule zitakazoshiriki mashindano ya UMISSETA Copa Coca-Cola wakati
wa uzinduzi wa mashindano hayo mwishoni mwa wiki.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla pamoja na maofisa wa kampuni ya
Coca-Cola wakipasha mwili kwa mazoezi kabla ya uzinduzi wa mashindano
hayo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akikagua baadhi ya timu za
wanafunzi wakati wa uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA Copa Coca Cola
katika uwanja wa Sokoine mwishoni wa wiki
Wanafunzi
kutoka shule mbalimbali za sekondari wakifanya mazoezi kwa
kushirikiana na wachezaji wa Mbeya City wakati wa uzinduzi wa
mashindano ya Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya
mwishoni mwa wiki.
Wanafunzi wakionyesha umahiri wa kusakata kabumbu wakati wa uzinduzi wa mashindano katika uwanja wa Sokoine mwishoni mwa wiki.
Michezo
ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari-UMISSETA Copa Coca- Cola kwa
Mkoa wa Mbeya imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki katika uwanja wa
Sokoine na uzinduzi huo ulionogeshwa na wachezaji wa timu ya soka ya
Mbeya City ambao walishiriki kufanya mazoezi na timu za wanafunzi na
kutoa ushuhuda wa michezo hiyo ilivyoibua vipaji vyao.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla,ambaye alikuwa mgeni rasmi anataka
kuwaona vijana wengi wakishiriki mazoezi na michezo mbalimbali kwa kuwa
michezo kama ilivyo hii ya UMISSETA Inaibua na kukuza vipaji pia sekta
ya michezo bado inazo fursa nyingi za kujiajiri.
Alisema
kampuni ya Coca- Cola imeonyesha njia kwa kudhamini michezo hii na
kutoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini michezo ya vijana
kwa kuwa ndio tanuru la kuwaandaa wachezaji na kuibua vipaji.
‘’Leo hii tunaona hawa vijana wa Mbeya City wapo hapa kutoa ushuhuda
wao, wanapokea mpunga (mshahara) wa maana lakini chimbuko lao wametokea
kwenye michezo hii ya Copa Coca- Cola.
Naamini
kupitia michezo hii Mbeya tutapata wachezaji wengi zaidi’.Alisema.
Ofisa Msaidizi Masoko wa Coca- Cola Pamela Lugenge, alisema lengo la
kampuni ya Coca Cola kuuungana na Serikali kupitia UMISSETA ni kuona
wanaibua vipaji vingi vya vijana walioko shule za sekondari ambako
wanaamini ndiko chimbuko la kupata timu ya taifa na klabu mbalimbali
nchini.
“Tumeamua
kuanzia kwenye mizizi ngazi ya chini kabisa, tunaamini huku ndiko
vipaji viliko lala, tunataka kuibuwa akina Mbwana Samata wengi zaidi
kuanzia huku, ndio maana tumejikita zaidi, na tunagawa vifaa vya michezo
kwa shule zote, tumeanza na shule hizi 39 za jiji la Mbeya na baada ya
uzinduzi huu sasa tunakwenda kwa wilaya zote kutoa vifaa hivi,” alisema
Lugenge.
Mchezaji
wa Mbeya City, Medson Mwakatundu,akiongea kwa niaba ya wachezaji
wenzake walioibuliwa na UMISSETA alisema michezo hii ni muhimu sana
iwapo Tanzania tunataka kuwa na wanamichezo wazuri kwa kuwa inaibua na
kukuza vipaji na alitoa wito kwa vijana kushiriki michezo kwa kuwa inazo
fursa nyingi za ajira na kutangaza taifa.
SHARE
No comments:
Post a Comment