Baada ya ukame
kumuandama, Mtanzania Mbwana Samatta ameamka baada ya kuifungia timu
yake ya KRC Genk bao la ushindi,Samatta amefunga bao la pili wakati Genk
ikiigaragaza Eupen kwa mabao 2-1 katika mechi ya ya kutafuta timu
itakayocheza Europa League msimu ujao.
Nahodha huyo wa Taifa
Stars alifunga bao hilo katika dakika ya 28 baada ya kupokea pasi ya
Thomas Buffel, akaupita msitu wa mabeki kwa kasi kabla ya kuukwamisha
mpira wavuni.
Kabla ya hapo, Genk ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Jere
Uronen katika dakika ya 18 akiunganisha basi nzuri ya Samatta hata
hivyo Eupen walipata bao la kufutia machozi dakika ya 76 likifungwa na
Mnigeria Onyekuru
Kwa ushindi huo, Genk inaendelea kuongoza Kundi B hatua ya play-off ikiwa na pointi 19 na kufuatiwa na Lokeren yenye ponti 10.
Kwa ushindi huo, Genk inaendelea kuongoza Kundi B hatua ya play-off ikiwa na pointi 19 na kufuatiwa na Lokeren yenye ponti 10.
SHARE
No comments:
Post a Comment