Wasichana walioshikwa mateka wakipanda helikopta ya jeshi |
NA K-VIS BLOG/Mashirika ya
Habari
WASICHANA 82, waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram nchini Nigeria
wakiwa bwenini kwenye shule moja ya Chibok nchini humo, kiasi cha miaka mitatu
iliyopita, wameachiwa huru Mei 7, 2017.
Wasichana hao wameachiwa kwa
kubadilishana na viongozi watano wa Boko Haram na ni matokeo ya majadiliano ya
miezi kadhaa yaliyohusisha wapatanishi toka mabara mawili.
Hata hivyo, wasichana hao ambao wakati
wanachukuliwa mateka walikuwa ni wanafunzi, wameacha wenzao kadhaa bado
wakishikiliwa. Boko Haram iliwachukua mateka jumla ya wasichana wa shule 276
wakiwa kwenye mabweni ya shule mnamo Aprili, 2014.
Kuachiwa huru kwa wasichana hao, kuna
fuatia majadiliano yaliyoratibiwa na Mustapha Zanna ambaye anaendesha kituo cha
yatima huko Maiduguri ambaye awali alikuwa mwanasheria wa mwasisi wa kundi hilo
la Boko Haram, Mohammed Yusuf, lakini pia majadiliano hayo yaklihusisha
serikali ya Uswis na Msalaba Mwekundu.
Wakiwa kwenye pick-up ya Msalaba
Mwekundu, na wakiwa wamevalia T-shirts zenye nembo ya Msalaba Mwekundu,
walionekana wakipanda helikopta ya jeshi na kusafirishwa kwenda mji mkuu Lagos
kukutana na Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari.
SHARE
No comments:
Post a Comment