TRA

TRA

Wednesday, May 24, 2017

Vijana 10 wabunifu wa Afrika walioshinda tuzo za Uingereza

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Taaasisi ya kutoa tuzo za watu Wabunifu na waliofikia malengo kwenye nyanja mbalimbali duniani Global TED imetoa tuzo kwa vijana 10 wa kiafrika walioweza kufanikiwa kuleta ubunifu na maendeleo kwenye nchi zao.

Tuzo hizi hutolewa kila mwaka Uingereza na kwa mara ya kwanza Washindi watazungumza na vijana wengine katika hafla itakayofanyika Arusha Tanzania August 2017.

Kwa Afrika mashariki Mwanahabari mchunguzi Yasin Kakande kutoka Uganda ameweza kuingia kwenye list hii kwa kufanikiwa kupata habari za kiuchunguzi zinazohusu uvunjifu wa haki za binadamu kwa Wafanyakazi wa kiafrika kwenye nchi za mashariki ya kati (Middle East).

Mwanabailojia aliyegundua tiba ya fangas kwenye mwili wa binadamu Mennat El Ghalid kutoka Egpt amefanikiwa kushinda tuzo hiyo kama kijana aliyeleta mapinduzi kwenye sekta ya tiba na afya pia mtaalam wa computer Abdighani Diriye kutoka Somalia na Mchekeshaji Carl Joshua Ncube kutoka Zimbabwe  ni miongoni mwa waliopata tuzo hizo.
                   Mwanasayansi  Mennat El Ghalid kutoka Egypt

Mwanaharakati wa maji safi na salama Saran Kaba Jones kutoka Liberia

Mwanasheria na mwanamitindo Wale Oyejide kutoka Nigeria

Mwanaharakati wa makosa ya kivita Adong Judith kutoka Uganda

Mwanahabari mchunguzi Yasin Kakande kutoka Uganda

Mwanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja (LGBT) Katlego Kolanye kutoka Botswana

Mwanamuziki wa Regge Kasiva Mutua kutoka Kenya

Comedian Carl Joshua Ncube kutoka Zimbabwe

Mtaalamu wa Computer Abdighani Diriye kutoka Somalia

Mwalimu Robert Hakiza kutoka Congo

CHANZO: Millardayo

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger