Kamati ya Saa 72 imekaa kupitia mambo mbalimbali na moja ya uamuzi wake ni kuhusiana na Yanga kugoma kuingia vyumbani.
Mechi namba 231 (Yanga 2 Vs Mbeya City 1).
Timu zote mbili
hazikupita kwenye mlango rasmi wakati wa kuingia uwanjani katika mechi
hiyo iliyochezwa Mei 13, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hivyo, kila klabu imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na
kitendo hicho, uamuzi ambao umezingatia Kanuni ya 14(48).
Washabiki wa Yanga
walivunja uzio wa ndani (fence) wa upande wa Magharibi wakati wakiingia
uwanjani kusherehekea ubingwa wa timu hiyo. Hivyo, klabu ya Yanga
imeagizwa kulipa gharama za uharibifu huo uliofanywa na washabiki wake,
uamuzi ambao umezingatia Kanuni ya 42(3) ya Ligi Kuu.
Pia Yanga imepigwa
faini ya sh. 1,500,000 (milioni moja na laki tano) kwa kutoingia
vyumbani. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(8) ya Ligi Kuu. Vilevile
klabu hiyo imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na
kuonyesha vitendo vinavyoashiria ushirikiana. Adhabu hiyo imetolewa kwa
mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu.
SHARE
No comments:
Post a Comment