Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam-Tanzania, Stephen Lokonyo akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam wiki iliyopita, wakati wa uzinduzi
wa bima ya afya hapa nchini. Katikati ni Mkuu wa Bima ya Afya ya
kampuni hiyo, Christine Mungi na kulia ni Mkuu wa Fedha na Utawala,
Irene Godson.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Bima ya Britam-Tanzania imezindua bima ya afya inayolenga kuhudumia
makampuni makubwa, biashara ndogo na za kati (SMEs).
Bima
hii inajumuisha gharama za matibabu ya wagonjwa waliolazwa, vipimo vya
magonjwa mbalimbali pamoja na majeraha yaliyotokana na ajali kwa
waajiriwa wasiopungua 10. Bima hii itagharimu kati ya shilingi milioni 5
mpaka milioni 200.
Akiongea
katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo,Steven Lokonyo
alisema bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi mpaka
hosipitali, ushauri wa daktari, gharama za chumba maalumu cha uangalizi
(ICU), mazoezi ya viungo, tiba ya mionzi, pamoja gharama za upasuaji.
Pia
bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi kwa ndege au gari
kwenda hosipitali kupata huduma za matibabu, gharama za uchunguzi za
eksirei na uchunguzi wa kimaabara.
"Bidhaa
hii tunayoileta kwenye soko inakuja kuleta mabadiliko katika sekta ya
afya na itaenda mbali kusaidia biashara ndogo na za kati na makampuni
makubwa hivyo kukuza ustawi pamoja na uzalishaji wa wafanyakazi wao"
alisema Lokonyo.
Lokonyo
alibainisha pia kwamba bima hiyo ina faida za nyongeza kama vile tiba
ya ugonjwa sugu uliogunduliwa, magonjwa ambayo mtu anayo kabla ya kuanza
kutumia bima,UKIMWI na magonjwa mengine kama kisukari, kansa, magonjwa
ya figo, ukurutu, maumivu ya viungo, magonjwa ya ini na kadhalika.
Uzinduzi
wa bima hiyo umefanyika kwa kuzingatia uhitaji wa soko pia ni mkakati
wa kampuni kupanua biashara yake ya bima nchini kwa kuangalia makundi ya
watu ambayo yalikuwa hayajafikiwa na huduma za bima.
"Bima
hii imeanzinduliwa kwa kuangalia uhitaji wa biashara ndogo na za kati
pamoja na makampuni. Kampuni yenye wafanyakazi 10 sasa inaweza kupata
huduma ya bima ambayo kila mtu anajua afya ya wafanyakzi ni muhimu kwa
biashara yoyoye" aliongeza Lokonyo.
Takwimu
za hivi karibuni zimeonyesha kuwa matumizi ya bima nchini Tanzania ni
chini ya asilimia moja ya pato la taifa ambacho ni kiwango cha chini
ukilinganisha na nchi zilizoendelea na nchi nyingine nyingi za kiafrika.
Katika jitihada zake za kufikia watanzania wengi zaidi, Britam inapanua
matawi yake nchini ambapo kwa sasa wapo katika mikoa saba ya
Dar-es-salaam, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Mtwara, na Arusha.
Kampuni
ya bima ya Britam Tanzania amabayo ilijulikana kama kama 'Real
Insurance' hapo mwanzo ni kampuni tanzu ya 'Britam Holdings' ambayo
inatoa huduma mbalimbali za kifedha katika bima, usimamizi wa mali, na
benki.
SHARE
No comments:
Post a Comment