Wa
kwanza kushoto ni Muasisi wa Tanzania Tour Guide Awards Sadock
Mugetta, aliyepo kushot kwake ni Katibu wa Freelance Guides Society of
Tanzania(FGST )anayefuata ni mjumbe wa wakiwa katika maonyesho
ya (3)Utalii ya Kilifair katika uwanja wa Chuo cha Ushirika
Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Na.Vero Ignatus Kilimanjaro.
Wito umetolewa kwa waongoza watalii nchini kutoa
ushirikiano ,kuwapendekeza watakaoingia katika kinyang'anyiro cha
kumtafuta mshindi wa Tuzo ambayo imeandaliwa kwaajili ya kumpata
Balozi atakaewawakilisha waongoza utalii nchini Tanzania,Afrika ya
Mashariki na Kati .
Akizungumza na blog hii Muasisi na mwenyekiti wa Tuzo
hiyo Sadock Mugetta amesema kuwa tuzo inafahamika
kama TANZANIA TOUR GUIDE AWARDS ambapo
mwaka jana ilikuwa imegawanyika katika vipengele vya
kumtafuta muongoza watalii bora wa Mlima,Safari pamoja na Wapagazi,ila
mwaka huu wameongeza vipengele viwili ambavyo ni Muongoza utalii wa
Utamaduni pamoja na Mpishi bora.
Sadock amesema kuwa wameamua kuwepo kwa Tuzo hiyo
kutokana hali halisi iliyopo ya ugumu wa kazi wanayoifanya waongoza
watalii (Mabalozi) ili mshindi atakayepatikana atawawakilisha
katika mambo yao ambayo wanataka Serikali iyafahamu,pamoja na wageni
mbalimbali waitambue Tanzania pamoja na vivutio vya Utalii
vilivyopo.
Ameongeza kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma
ya utalii hapa nchini waongoza Watalii hawajawahi kupewa
kipaumbele, hivyo ni vyema Serikali ikatambua kuwa muongozaji watalii
huwa anatumumia 99% ya muda wao kukaa na mgeni awapo
nchini na anapewa taarifa zote sahihi na muhimu hadi anaondoka
nchini.
"Ikumbukwe kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma hii ya utalii waongozaji hawajawahi kupewa kipaumbele wakati anatumia 99%ya muda wake na mgeni akiwa hapa nchini ,anahakikisha mgeni yupo salama,anahakikisha mgeni anapata taarifa zote sahihi hadi anaondoka nchini,muongozaji huyu anafanya kazi yake kama mwalimu,Daktari pale mgeni anapopata taizo anampatia huduma ya kwanza,mpishi,mpatanishi na Balozi mwaminifu".alisema Sadock.
Kwa
upande wake Katibu wa Waongoza watalii wa kujitegemea Ally
Mtemvu amesema kuwa hakuna mgeni anayekuja nchini kufanya utalii
pasipokuwa na muongozaji amesema tuzo hiyo inawashirikishwa
makampuni yote ya utalii ,wadau wa utalii KIATO,TATO, pamoja
KGA,TTGA,FGST,KTAS,TTG,KILIMERU,TPO,MMPA,NCPG na NMPA
" Hivyo
tunaiomba Wizara ya Utalii na Maliasili watuunge mkono kuhakikisha
kuwa tuzo hii ya Afrika Mashariki na Kati zinakuwa bora zaidi kwakuwa
tumewatangulia na imeasisiwa nchini Tanzania "alisema Ally.
Aidha
Tuzo hii ilizinduliwa rasmi mwaka 2016 mkoani Arusha ambapo mgeni
rasmi alikuwa Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Anjelina Madete,ambapo mwaka huu 2017 itafanyika jijini Dar es salaam
kwenye maonyesho ya SITE october 13-15,2017 ambapo mgeni rasmi
atafahamika hapo baadae.
Mwisho wa mapendekezo ya majina ni tarehe
30/6/2017
SHARE
No comments:
Post a Comment