TOKYO- MJI Mkuu
wa Angola, Luanda, umechukua nafasi ya kwanza kama mji ghali zaidi duniani kwa
wataalamu na kuupiku mji wa Hong Kong ambao umeshika nafasi ya pili.
Kwa mujibu
wa utafiti uliofanywa na Shirika la Mercer, mji huo unakuwa ghali zaidi kuliko
miji yote duniani kulingana na gharama za kuishi katika mji huo. Miji ya Tokyo,
Zurich na Singapore pia nayo imefanikiwa kuwepo katika nafasi tano za mwanzo.
Mji wa
London umeporomoka hadi nafasi ya 30, kutokana na kushuka kwa thamani ya pauni.
Utafiti huo wa kila mwaka, huangazia masuala kadhaa kando na gharama ya kukodi
nyumba.
Utafiti huo
huangazia gharama ya vitu 200 kwa kila mji, ikiwemo nyumba, usafiri, mavazi,
chakula na burudani.
SHARE
No comments:
Post a Comment