Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako
alifanya ziara ya ghafla katika
shule Mkoani Iringa. Alitembelea shule zinazo fundisha watoto wenye
mahitaji maalum za Makala Wilaya ya Mfundi, Shule ya viziwi Mtwivila,
Shule ya sekondari ya wasichana Mtwivila na shule ya sekondari ya
Lugalo. Nia ya ziara ni pamoja na kukagua vifaa vya kufndishia ambvyo
serikali imetoa. Pia alipta fursa ya kusalimia wanafunzi na walimu.
Katika ziara hiyo aliongzana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina
Masenza, Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Bi wamoja Ayoub, Wakuu wa
wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Jamhuri David na Iringa Mheshimiwa Richard
Kasesela. Pia wabunge waheshimiwa, Ritta Kabati, Zainab Mwamwindi na Mch
Peter Msigwa
Mheshimiwa Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya
Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela kushoto ni Mbunge wa jimbo la Iringa
mjini Mchungaji Peter Msigwa.
Mheshimiwa Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza pamoja na viongozi
mbalimbali mkoani Iringa wakifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya
maalum ya viziwi mkoani humo
Mheshimiwa Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na Mbunge wa Iringa
mjini Mh. Mchungaji Peter Msigwa katika Shule ya Viziwi, kulia ni
Mbunge Viti Maalum Mhe Zainab Mwamwindi akisikiliza na katikati ni
Mbunge wa viti Maalum Iringa Mh. Ritha Kabati.
Mheshimiwa Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na Mh. Ritha Kabati
akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi
Profesa Ndalichako nawanafunzi wa Iringa Girls
Profesa Ndalichako akiongea na wananfunzi wa Shule ya sekondari Lugalo kidato cha 5
SHARE
No comments:
Post a Comment