Msanii
mkongwe wa Hip hop nchini, Afande Sele ambaye hivi karibuni amerudisha
kadi yake ya chama cha ACT - Wazalendo, na kuamua kubaki mwananchi wa
kawaida huku akiunga mkono kile kinachofanywa na Rais Magufuli, amesema
kwa sasa ana imani iko salama
Afande
Sele amesema moja ya sababu ambayo ilimfanya aingie kwenye siasa ni
mambo yasiyofaa yaliyokuwa yakifanywa na serikali za awamu zilizopita,
huku akiamini anaweza akaleta mabadiliko, lakini kwa sasa haina haja ya
yeye kuendelea kufanya hivyo, kwani uongozi uliyopo upo makini.
"Nina
amini kabisa mambo mengi ambayo nayatazama kwenye nchi yanavyoendelea
sina shaka nayo kabisa kwa sasa. Sababu kubwa iliyonipelekea niingie
kwenye siasa ni kutokana na utawala mbovu uliyokuwa katika awamu
zilizopita. Nchi ilikuwa kama Kambale hakuna mtu ambaye anaweza kukemea
jambo baya kwa kuwa kila mmoja alijiona mkubwa , nchi ilikuwa inajiendea
hovyo hovyo tu. Ndiyo maana nikaamua kuingia kwenye siasa lakini sasa
kidogo uliyopo naona unafanya niliyokuwa nayataka", alisema Afande Sele.
SHARE
No comments:
Post a Comment