Msanii wa muziki kutoka Visiwani Zanzibar, Baby J amefunguka kuwa hana mpinzani katika muziki anaoufanya.
Baby
ameeleza kuwa hajawahi kuwa na mpinzani katika muziki anaofanya yeye,
Licha ya kuwa miaka ya zamani alikuwa akishindanishwa na mwanamuziki
Sainaj kutokea huko huko, mrembo huyo amekana kuwa na mpinzani.
“Kwanza
sijawahi kuwa na mpinzani, kwa sababu siku zote unakuwa unajiona wewe
mwenyewe huoni cha mbali mimi navyo jiona yani kwanza nime zaliwa
Zanzibar, nimefumbua macho Zanzibar, hao wote wanaojiita wapinzani ndiyo
nimewepokea hapa Zanzibar, so siamini kama nina mpinzani,” amesema
mrembo huyo ambaye hivi karibuni ameshirikishwa kwenye ngoma mpya ya
Kasssim Mganga.
Pia ameongeza kuwa moja ya sababu zinazowafanya wasanii wa kike kuwa wa chache kisiwani humo ni kutokana na kutokujiamini.
SHARE
No comments:
Post a Comment