Kijana Emmanuel Ernest wa kitongoji cha Ilolo, Mvumi Misheni wilaya ya
Chamwino Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kukanyagwa na tembo
huku mwingine akijeruhiwa vibaya baada ya tembo huyo kuvamia mashamba ya
zabibu.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema tembo huyo alikuwa akitafuta maji
majira ya alfajiri hivyo baadhi ya wanakijiji baada ya kumuona
walikusanyika na kupiga mayowe, kitendo kilichomfanya mnyama huyo
kukasirika na kuanza kuwafukuza kabla ya kumkuta marehemu Emanuel akiwa
na mdogo wake wakichimba mitaro ya mizabibu na kumkanyaga kifuani na
kumvunja mbavu nne na kusababisha kifo chake.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mvumi Misheni, Peter Songoro,
amethibitisha kupokea majeruhi wawili, akiwemo marehemu na mdogo wake
Amani Joseph ambaye alikanyagwa mgongoni na kisha utumbo kutoka nje,
kabla ya Emmanuel kufariki baadaye wakati akipatiwa matibabu.
SHARE









No comments:
Post a Comment