NA
K-VIS BLOG/MASHIRIKA YA HABARI
Romelu
Lukaku ameonyesha cheche zake baada ya kutupia mawili kati ya mabao manne
ambayo Manchester United wameshinda dhidi ya West Ham United wakati wa mchezo
wa ufunguzi wa ligi kuu ya Uingereza (VPL) uliopigwa uwanda wa nyumbani Old Trafford.
Lukaku
ambaye amesajiliwa na Manchester United kwa kitita cha Pauni za Uingereza
Milioni 75 alionyesha kuwa “anatosha” ambapo West Ham, (The Hammers), kama
wanavyoitwa ncbini humo, ilionyesha kupwaya kabisa mbele ya Mashetani hao
wekundu kutoka jiji la London.
Manchester
United walianza kushika usukani mapema ambapo ingizo hilo jipya, Lukaku akitayarishiwa
mipira murua na kiungo Nemanja Matic ambaye alionekana kuwa ndio chachu ya
mashambulizi ya Manyuuu kila wakati.
SHARE
No comments:
Post a Comment