WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, amesema, uwekezaji mkubwa
utakaofanywa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC baada ya
kuorodheshwa rasmi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) jana
utasaidia kuongeza mapato ya Serikali na kuwezesha wananchi.
Kampuni
hiyo jana ilijiorodhesha hisa zake DSE baada ya kuuza asilimia 25% ya
hisa zake ambapo kiasi cha shilingi bilini 476 kimefanikiwa kukusanywa.
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya uorodheshaji wa hisa hizo, Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, alisema uoredheshwaji huo ni hatua
muhimu ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“Mgawanyo
wa hisa zilizouzwa kwa umma umefanyika kwa kutoa kipaumbele kwa
wawekezaji wa ndani ya Tanzania ambapo wamepata aslimia 100% ya maombi
yao ya waliofanya katika ununuzi wa hisa zilizouzwa kwa umma na hivyo
hivyo wawekezaji wa ndani kupata asilimia 60% na wawekezaji wa kimataifa
asilimia 40%,”.
Waziri
Mpango alisema kipaumbele kimetolewa kwa wawekezaji wa ndani ili
kuwezesha Watanzania kuwa washiriki katika maendeleo ya uchumi wa nchi
yao badala ya kuachwa pembeni ya mageuzi na maendeleo ya kiuchumni
yanayotokea hapa nchini.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao
alimwambia Waziri Mpango kuwa fedha zilizokusanywa zitatumika kufanya
uwekezaji zaidi na hivyo kuwafanya wawekezaji wapya kunufaika na
uwekezaji wao ndani ya Vodacom Tanzania.
“Tutaendelea
kufanya uwekezaji mkubwa na wenye tija kwa ajili ya wanahisa wetu.
Vodacom ndiyo kampuni ya simu za mkononi inayoongoza na kupitia
uwezeshaji huu wa kimtaji tunatarajia kukuwa zaidi,”alisema
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na
Dhamana Dk John Mduma alisema mafanikio hayo yanaleta chachu ya
maendeleo na mageuzi katika sekta ya masoko ya mitaji na fedha hapa
nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (kulia)akipiga kengele
kuashiria kuorodheshwa rasmi kwa hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania PLC
katika Soko la Hisa la Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao na Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE
Moremi Marwa.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (kulia) akimpongeza
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (katikati)
kuhusiana na kufanikisha kuorodheshwa rasmi kwa hisa za kampuni yake
katika Soko la Hisa la Dar es Salaam jana.Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu
wa DSE Moremi Marwa.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (wapili kulia) Mwenyekiti
wa bodi ya soko la hisa, John Mduma (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa
DSE Moremi Marwa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania
PLC,Ian Ferrao akifafanua jambo wakati wa Uzinduzi wa hafla ya
kuorodheshwa rasmi kwa hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania PLC katika
Soko la Hisa la Dar es Salaam jana.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiongea wakati wa hafla
ya Uzinduzi wa kuorodheshwa rasmi kwa hisa za kampuni ya Vodacom
Tanzania PLC katika Soko la Hisa la Dar es Salaam jana. Katikati ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE Moremi Marwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao.
SHARE
No comments:
Post a Comment