Rais
mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassani Mwinyi,akipata maelezo ya
jitihada za kampuni ya TBL Group kupambana na ajali za barabarani kutoka
kwa Ofisa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Amanda Walter kwenye tamasha la usalama barabarani lililofanyika jijini Dar e salaam mwishoni mwa wiki (kulia) mwenye kofia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni.
Daktari wa macho katika gari la Zahanati mwendo laTBL Group, Nestory Massawe (kulia) akimpima macho mwananchi Omar Hussein wakati wa tamasha la usalama barabarani katika uwanja wa Taifa anayeshuhudia (kushoto) ni Ofisa Mawasiliano wa kampuni hiyo ,Amanda Walter
Baadhi ya madereva wa bodaboda wakipata mafunzo ya usalama barabarani kutoka kwa maofisa wa TBL wakati wa tamasha hilo
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria tamasha hilo.
NA MWANDISHI MAALUM
Kampuni ya TBL Group imeeleza
dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine
nchini kuunga mkono kampeni za usalama barabarani lengo likiwa
ni kupunguza ajali nchini ambazo zimekuwa zikisababisha vifo vya watu
,kuacha wananchi wengi wakiwa walemavu na kusababisha hasara mbalimbali.
Akiongea wakati wa tamasha la Usalama barabarani 2017,lililoandaliwa na serikali kupitia Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani na kufanyika katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ,Afisa
Mawasiliano wa TBL Group,Amanda Walter,alisema suala la usalama wa
barabarani kampuni inalipa kipaumbele mkubwa na ndio maana imekuwa
ikijihusisha nalo kama moja ya agenda ya kusaidia huduma za kijamii.
Alisema
kuwa kampuni imekuwa moja ya wadau wakubwa wa kudhamini wiki ya Nenda
Kwa Usalama Barabarani mwaka hadi mwaka sambamba na kudhamini
mafunzo,vitendea kazi na wafanyakazi wake kushiriki katika kutoa elimu ikiwa ni ufanikishaji wa moja ya mkakati wa kampuni wa kutokomeza matukio ya ajali za barabarani na maeneo ya kazi.
“Linapokuja suala la usalama kampuni inalizingatia kuanzia usalama wa ndani katika maeneo ya kampuni hadi usalama wa barabarani kwa ajili ya watu wote na ndio maana tumekuwa tukiunga mkono kampeni hizi ikiwemo kuwamasisha madereva wasiendeshe vyombo vya moto wakiwa wametumia vinywaji vyenye kilevi”.Alisema Walter.
Aliongeza
kuwa hivi sasa kampuni hiyo imekuja na mkakati mkubwa wa kuendesha
mafunzo ya kuhamasisha jamii Unywaji wa Kistaarabu “Tukiwa
kampuni inayotengeneza vinywaji vyenye kilevi tunalo jukumu pia
kuhamasisha jamii kutumia vinywaji hivyo vizuri ili utumiaji wake
usilete madhara mengine kwenye jamii”
Mwaka
jana TBL Group ilikuwa mmoja wa wadhamini wa Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani iliyofanyika kitaifa mkoani Geita ambapo iliwezesha idadi
kubwa ya madereva kupima afya zao kupitia huduma ya Zahanati Mwendo pia
imekuwa ikiendelea kudhamini kampeni hizo kwenye ngazi za mikoa ikiwemo
kudhamini mafunzo ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za
msingi.
Katika tamasha hilo gari la Zahati Mwendo la TBL Group lilikuwa moja ya kivutio kikubwa kwa wananchi walioudhuria ambapo baadhi yao waliweza kupata huduma za ushauri wa kiafya na kupimwa macho.
Akiongea baada
ya kutembelea mabanda ya maonyesho ya taasisi mbalimbali katika tamasha
hilo,Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh.Ali Hassan Mwinyi,aliwapongeza
wadau wote ambao wanashiriki kampeni za kutokomeza matukio ya ajali
nchini na kutoa wito kuwa serikali ikishirikiana na taasisi zisizo za
kiserikali kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii mafanikio yatapatikana kwa haraka na taifa kuzidi kusonga mbele kwa haraka.
SHARE
No comments:
Post a Comment