TRA

TRA

Friday, September 1, 2017

Mtoto wa Rais Jacob Zuma akanusha madai ya ufisadi

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Mwanawe Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, amekanusha madai kuwa amehusika katika kashfa ya ufisadi na kuwa na uhusiano na mfanyibiashara mmoja mwenye utata.

Duduzane Zuma ameiambia BBC kuwa, hakuna "ambacho hakijasemwa" kuhusiana na mshirika wake wa kibiashara na familia ya Gupta.
 Duduzane Zuma ni mmojawepo wa watoto 21 wa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini

Barua pepe ambayo inahusiana na familia ya Bwana Zuma na ile ya magupta na kuanzisha uchunguzi ambayo itaonyesha uwezekano wa kuingiliwa kisiasa.

Rais Zuma na familia ya Magupta, mara kwa mara yamekanusha kuhusika na jambo lolote baya.

Katika mahojiano ya kipekee yaliyofanywa na mwaandishi wa BBC Milton Nkosi, Duduzane Zuma amesema kuwa, uhusiano wake na familia tajiri ya Magupta, hauna mambo mengine zaidi kwani yeye ni "mtu mzuri anayependwa na wengi".

"Siamini kuna kitu wanachohitaji kutoka kwangu," alisema huku akiongeza kuwa: "Wananipenda. Na mimi pia nawapenda."
Duduzane Zuma, ambaye ni mmojawepo wa watoto 21 wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, anasisiiza kuwa "si mfisadi".
"Binafsi sijawahi husika na biashara yoyote ya ufisadi," amesema.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger