Askari Polisi wakiwa tayari kwa
kazi katika moja ya magari 18 yaliyokamilika kwa ukarabati kati ya
magari 26 yaliyopelekwa kwenye gereji ya RSA mjini Moshi na Mkuu wa mkoa
wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa matengenezo makubwa wakati
alipoyakagua Septemba 15, 2017 mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Paul Makonda akikagua moja ya magari 18 kati ya 26 ya polisi Dar es
salaam yaliyopelekwa mjini Moshi katika gereji ya RSA kwa matengenezo
makubwa Mkuu wa mkoa huyo ameyakagua magari hayo na atakabidhiwa magari
18 ambayo yamekamilika.
Baadhi ya magari ambayo tayari yamekamilika kwa matengenezo.
………………………………………………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe.Paul Makonda Septemba 15, 2017 ametembelea na kukagua ukarabati mkubwa wa magari 26 ya polisi
yaliyopelekwa mkoani Kilimanjaro yakiwa mabovu ili yafanyiwe ukarabati
na kubadilishwa muundo wake na kuwa maalum kwa kazi za kipolisi.
Mhe. Makonda ameambiwa tayari magari 18 yamekamilika
kwa kufungwa vifaa
mbalimbali ikiwemo matairi mapya, taa,vioo, kunyooshwa bodi na kupakwa rangi ikiwa ni pamoja na kuandikwa maandishi ya polisi.
Mhe. Makonda amesema ameridhishwa na kazi iliyofanyika na kwamba atakabidhiwa magari hayo mwanzoni mwa mwezi Oktoba
Amesema Magari hayo yenye mwonekano kama yale ya UN yatakuwa
na uwezo wa kubeba Askari tisa nyuma wakiwa wamekaa ambapo askari watatu
watakuwa wakitazama nyuma, watatu kushoto, watatu kulia na mmoja mbele
na wote wakiwa wamebeba silaha.
Aidha Makonda amesema kupatikana kwa magari hayo yatasaidia kupunguza vitendo vya Uhalifu kwa Wananchi.
RC Makonda amesema kuwa lengo lake ni kuona hakuna Mwananchi yoyote anaeibiwa au kuporwa kitu.
Hata hivyo amesema Baadhi ya Askari walikuwa wakipoteza
maisha na kuporwa Silaha kutokana na aina ya Magari waliyokuwa wakitumia
kutowapa uwezo wa kukabiliana na wahalifu hivyo Magari hayo yatamaliza
matukio hayo.
Ameishukuru kampuni ya RSA Limited kwa kumuunga mkono kwa
kujitolea kukarabati Magari 56 ya Jeshi la Polisi kwa kuyafanya kuwa ya
kisasa na mapya.
Sanjari na hayo amesema Magari hayo yataenda kufanya Doria kwa masaa 24.
Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya RSA Bwana Manmohan Bhamra
amesema kwa sasa Magari hayo ni sawa na Mapya kwakuwa yamewekwa vifaa
vipya.
Amesema Magari yote watayakabidhi kwa wakati iliyakaongeze tija katika kuimarisha Ulinzi na Usalama kwa Wananchi.
SHARE
No comments:
Post a Comment